Telegram ni moja kati ya mitandao mikubwa sana ya kijamii na ni moja kati ya ile ambayo inaaaminiwa kuwa na mambo mengi kwa watumiaji.
Mojawapo ni kwamba Telegram ina usalama na ulinzi wa hali ya juu kabisa kwa watumiaji wake na sifa hiyo imekua ikiwekwa wazi wazi na watu mbalimbali.
Unaweza ukaanza kujiuliza kwa sasa mbona kipengele cha Stories sio cha kukishangaa maana karibia mitandao mingine yote tayari ina kipengele hicho? Je Telegram wao walikua wapi wakati wote huo?
Mkuu wa Telegram Bwana Pavel Durov yeye anasema watumiaji wa mtandao huo wamekua wakiomba kuletewa kipengele hicho kwa miaka na sasa amewasikia vya kutosha.
Kipengele cha Stories kinatarajiwa kuanza kupatikana katika mtandao huo tarehe za mwanzo mwanzo kabisa za mwezi wa saba mwaka huu.
Ni wazi kwanza mtandao umeweka wazi kabisa kwamba mwanzoni hawakutaka kabisa kuongeza kipengele hiko kwa sababu kinapatika karibia kila katika mtandao wa kijamii.
Hapa ndipo nguvu ya watumiaji inapokuja, sasa wameshasikilizwa na kwa hara haraka hili ni jambo zuri maana ushindani kati ya Telegram na mitandao mingine yenye huduma kama hii inaongezeka.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment? Je hii umeipokeaje? Je unatumia mtandao wa Telegram, kipengele hiki kipya umekipokeaje?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.