PowerPoint ni moja kati ya program maarufu sana kutoka Microsoft na ni moja kati ya zile zinazojulikana kama MICROSOFT OFFICE. Licha ya umaarufu wake wa kuwa ya kutumika zaidi katika kufanya maonyesho na hii mara nyingi inakuaga kwa shuguli za kiofisi.
PowerPoint kwa kawaida huwa inakuwa na zana mbalimbali ambazo zinamuwezesha mtumiaji kuandaaa onyesho lake vizuri. Kunakuwa na zana pamoja na vipengele mbali mbali vya kumsaidia, mara nyingi watu hawatumii vipengele na zana hizi kwa sana.Hata hivyo vipengele vipya vya Designer Na Morph! katika PowerPoint vinatarajiwa kuifanya PowerPoint kuwa ya aina yake.
Kipengele Cha Morph (Morph tool) kinamuwezesha mtumiaji wa programu hii kuweza kutengeneza ‘Animation’ nzuri kwa urahisi kabisa. ‘Animation’ hizo zinaweza kuwa za picha, maneno na pia hata kuongeza mbwembe katika maumbo ya 3D. Kwa upande wa PowerPoint Morph ndio kipengele chake kipya zaidi katika masuala ya kutengeneza vitu (maumbo, maneno n.k) yanayotembea/kusogea.
Designer chenyewe kipo Spesheli kwa ajili ya picha. hapa utaweza kupakia picha zako na kisha zitaweza kufanyiwa kazi.. Picha hizo zitahifadhiwa katika ‘Microsoft Cloud’ na kisha mtumiaji anaweza akachagua picha anazotaka labda kati ya zile nyingi na pia anaweza chagua mpangilio wa picha hizo. Watumiaji wa hii itabidi wakubali ili picha zao ziweze kuwekwa katika ‘Microsoft Cloud’ tayari kwa kufanyiwa mchakato
Pia Microsoft iko katika mchakato wa kuweka kipengele ambacho kitakuwa kinaongeza rangi kiautomatiki katika ukurasa (slide. Hii inamaanisha PowerPoint itaweza chagua rangi ya kuweka katika ukurasa kulingana na rangi ambazo zimepatikana labda katika picha aliyoweka mtumiaji. Hii inamaanisha kuwa mtumiaji ataweza kusevu mda wake ambao angeutumia kuchagua na kuweka rangi yeye mweneyewe.
Vipengele vya Morph na Designer vitakuwa vinatumiwa na watumiaji wa ‘Office 365’ pekee ambao wanatumia windows 10 au wale wanaotumia Microsoft PowerPoint katika Desktop zao.
Huduma hii inatarajiwa kaunza kufika mwaka 2016, lakini kuna programu maalamu ‘Office Insider program’ imeandaliwa kwa watu ambao wangependa jaribu kuitumia mapema, hivyo basi wanatakiwa kujiunga katika ukurasa huu