Mara nyingi inaweza ikakubidi ubadilishe mfumo wa faili la wimbo au video kutoka aina moja kwenda aina nyingine ili uweze kutumia katika kifaa chako husika – simu, tableti n.k.
Kutafuta programu inayofaa na isiyokuwa na matatizo hasa hasa ya matangazo mengi au kukuwekea programu nyingine chafu kwenye kompyuta yako inakuwaga ni changamoto. Je ulikuwa unafahamu ya kwamba VLC inaweza kufanya kazi hiyo pia?
Kama tayari kwenye kompyuta yako una programu ya kuchezesha mafaili ya video na muziki ya VLC basi hauitaji programu nyingine kabisa.
VLC ni programu ya bure yenye uwezo mkubwa pia wa kubadilisha mafaili kutoka kwenda mfumo mmoja kwenda mfumo mwingine; mfano kutoka .AVI kwenda .MP4 au .MP3 n.k.
Hatua ya kwanza
Fungua programu ya VLC
Hatua ya pili
Bofya eneo la Media -> Convert/Save, Kisha bofya ‘Add‘ na uchague faili unalotaka kulibadilisha mfumo (covert)
Hatua ya tatu
Hapo hapo eneo la Convert pia linaonekana, mbele ya ‘Profile‘ bofya na uchague mfumo mpya unaotaka faili hilo liwe
Hatua ya nne
Kwenye eneo la ‘Destination‘ kunamaanisha eneo ambalo faili jipya litawekwa, unaweza pia kulipa jina jipya. Bofya ‘Start‘ na VLC itaanza kazi ya ku’covert faili husika.
Kutegemeana na ukubwa wa faili lako basi kazi hiyo inaweza ikafanyika ndani ya muda mfupi au dakika kadhaa. Mara nyingi video ndio zinachukua muda mrefu.
Ingawa VLC inauwezo wa kufanya vitu vingi ni kwamba tuu hawajitangazi sana kwa kujipa sifa kama huduma zingine hasa zile zinazotafuta pesa (yaani za malipo) katika kufanya haya.
Unaweza kupakua/download programu ya VLC kutoka hapa -> http://www.videolan.org
One Comment