fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

apps Google Drive Maujanja Teknolojia

Zuia watu kukusambazia vitu vyao kupitia Google Drive

Zuia watu kukusambazia vitu vyao kupitia Google Drive

Spread the love

Imekuwa ni jambo rahisi sana kutuma/kupokea kitu kupitia Google Drive hivyo kufanya mawasiliano kufanyika kwa njia ya haraka lakini inawezekana pia unachukizwa na kile ambacho mtu ameamua kukutumia huko, sasa umepewa rungu la kuweza kuzuia watu kukusambazia vitu vyao.

Utakubaliana na mimi kwamba uwepo wa Google Drive umepunguza kwa kiasi kikubwa namna gani ya kupata nyaraka zetu iwapo unataka kuiona/kuifanyia kazi lakini umeihifadhi kwenye kompyuta sehemu ambayo haiwezekani kuipata nyaraka husika wakati wowote na mahali popote.

Hata hivyo, kwa upande mwingine kuna watu wanaweza kukwa na mtindo wa kukushirikisha vitu vyao kupitia Google na wewe huvihitaji ama hupendezwi navyo. Fahamu ya kuwa Google Drive imwboreshwa na kumpa mtumiaji uwezo wa kumfungia uwezo wa kupokea vitu kutoka kwake. Fuata njia hizi iwapo unatumia simu au kompyuta ili kuweza kuzzuia kupokea vitu kutoka kwa mtu/watu ndani ya Goole Drive:

>Hatua za kufuata kupitia simu janja (iOS/Android). Mosi, fungua programu tumishi ya Google Drive kisha angalia upande wa kulia juu kabisa palipo na nukta 3 ndogo zilizofuatana kwa kwenda chini. Pili, bofya “Block” kisha weka barua pepe ya mtu unayetaka kumzuia (block). Tatu, bofya “Block” kukubali.

kukusambazia vitu vyao

Hatua za kufuata kama unatumia simu janja ili kuweza kuzuia mtu kukusambazia vitu vyake.

>Hatua za kufuata kupitia komyuta. Kwanza, tembelea drive.google.com, nenda kwenye faili husika kisha bofya kitufe cha pili  kiteuzi (mouse). Baada ya hapo bofya “Block” kisha weka barua pepe ya mtu unayetaka kumzuia (block). Mwisho, bofya “Block” kukubali.

kukusambazia vitu vyao

Hatua za kufuata iwapo unatumia kompyuta ili kuweza kuzuia mtu kukusambazia vitu vyake.

Kuruhusu kupokea vitu kutoka kwake tena inawezekana pia.

Iwapo utataka kumtoa mtu sehemu uliyemfungia ndani ya Google Drive kama unatumia rununu/kompyuta hatua za kufuata ni kufungua programu tumishi husika (Google Drive) ama tembelea drive.google.com, halafu nenda kwenye sehemu ya picha yako ya utambulisho>>Manage your Google Account>>People & Sharing>>Blocked. Utaona orodha ya watu wote uliowazuia na pembeni ya jina/barua pepe kuna neno “Remove” ukibofya hapo utakuwa umemuondoa “Kifungoni”.

kukusambazia vitu vyao

HAtua za kufuata kumwondoa mtu kwenye orodha ya watu uliowazua wasikutumia vitu vyao kupitia Google Drive.

Tufahamu kwamba unapomzuia mtu kwenye Google Drive mbali na wao kushindwa kukusambazia vitu vyao hata na wewe hutaweza kufanya hivyo (mpaka utakapo mtoa kizuizini), hataweza kufungua mafaili yako na wewe hutaweza kuona ndani ya kile ambacho alikutumia.

Inashauri kusubiri kwa dakika kadhaa kuweza kuruhusu kwa mabadiliko kuonekana. Iwapo unatumia Google Drive ya kazi/shule hairuhusu kuzuia mtu kwa kutumia akaunti yako.

Chanzo: Google Drive

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania