Gmail imekuwa ni chaguo la kwanza la wengi katika swala zima la matumizi ya barua pepe, licha ya hivyo bado mtandao una zaidi wa watumiaji bilioni moja.
Hilo likiwa katika akili yako, kumbuka unaweza kuutumia mtandao hup kwa urahisi kabisa kwa kutumia njia njia za mkato na ujanja ujanja flani ambao kwa namna moja au nyingine utakusaidia kuokoa muda.
ShortCut hizi zina jinsi ya kuziwasha kama ndio unakua unatumia kwa mara ya kwanza.
Jinsi Ya Kuziwasha
. Fungua Gmail kwa kutumia kompyuta yako
. Nenda katika uwanja wa Settings
. Katika eneo la General Settings shuk chini mpaka katika Keyboard ‘ShortCuts’ na kisha washa
. Shuka chini na kisha Sevu mabadiliko haya
ShortCuts Na Kazi Zake
1. Andika Barua Pepe Mpya – bonyeza ‘C’ kuandika mpya au ‘D’ kuandika mpya katika Tab nyingine
2. Search – bonyeza alama ya ‘/’ na kisha unaweza ukaandika maneno unayotaka kutafuta
3. Fungua Menu Ya More – bonyeza alama ya ‘.’ na kisha unaweza ukachagua machaguo chini ya menu ya more
4. Nenda katika barua pepe ya zamani – bonyeza ‘j’ wakati ukiwa unasoma barua pepe kwenda katika ile ya zamani
5. Nenda katika barua pepe mpya – bonyeza ‘K’ kwenda katika barua pepe mpya
6. Kujibu barua pepe – kumjibu kila mtu bonyeza ‘a’ ila kumjibu mtu mmoja mmoja bonyeza ‘r’
7. Kufuta barua pepe – bonyeza ‘Shift na #’ kwa pamoja
8. Kutuma Barua pepe- bonyeza ‘Ctrl na Enter’ kwa wakati mmoja
9. Kuweka link katika barua pepe – bonyeza ‘Ctrl na K’ kwa wakati mmoja
10. Ku’forwad barua pepe – bonyeza ‘f ‘ wakati umefungua barua pepe hiyo
Kwa kuwa hayo hapo juu ndio mambo ya muhimu zaidi ambayo huwa yanafanywa mara kwa mara na watumiaji wa mtandao wa Gmail ndio maana yamekuwa ya kwanza kuwekwa wazi wazi.
Ila kama bado unataka zaidi ya hayo unaweza ukatazama picha ya hapa chini kwa umakini kwani inaonyeza ‘shortcut zote’.
Je ulikuwa unayajua maujanja haya? Teknokona ndio jumba lako la habari na mujanja mbalimbali yanayohusu teknolojia. Ningependa kusikia kwako, niandikie hapo chini sehemu ya comment je hii umeipokeaje?