Ndio namaanisha Kope kabisa zile zinazokaa juu ya macho. Wengi najua watkua wameshtuka ila kumbuka wazungu wanatushtua kila siku kwa vitu ambavyo wanavizalisha ukizingatia na ukubwa wa Teknolojia ambao wanao.
Kope janja hizi zinajulikana kama F.Lashes, Kope hizi zimetengenezwa na bwana Tien Pham, ambae kwa sasa ana mpango wa kupeleka ubunifu wake mbele zaidi na kuanza kuuza kama bidahaa

F.lashes inajumuisha vitaa vidogo dogo sana (LED) ambavyo unaweza ukavivaa juu kidogo ya kope.Lakini kutakuwa na waya na kamtambo kadogo ambako katakuwa kama ndio kanaongoza vitaa hivyo. Mara nyingi kamtambo haka itabidi ukafiche, kwa mfano kwa wanawake wanapenda kuficha chini ya nyewele zao.
F.Lashes zipo za aina saba na zote zinautofauti wake na pia huwa zinajiwasha na kuzima kulingana na mwili wa mtu unavyosogea.

Kitu ambacho watu hawajakipokea kwa mikono miwili mpaka sasa ni ule waya ambao unatoka katika F.Lashes kwenda katika kamtambo kanakoongoza mfumo mzima. Wengi wametoa maoni kwamba kaondolewe na F.lashes zijitegemee zenyewe
Kama mafanikio yakitokea na nyaya ikaondolewa, bidhaa hii inaweza ikateka dunia kwa kiasi kikubwa sana. Bidhaa kama hizi zitakuwa zinavaliwa sana sehemu za starehe kama vile Club na kwenye sherehe mbali mbali.

Ningependa kusikia kutoka kwako, niambie hii imekaaje? kama bidhaa hii ingekuja bongo ungenunua? niandikie hapo chini sehemu ya comment.
Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!