fbpx

Zifahamu Huawei Honor 8X na 8X Max

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Mwezi Septemba ulikuwa ni simu baada ya simu tukiwa tumeshazifahamu rununu kadha wa kadha ambazo zilitoka na moja kati ya hizo ni Huawei Honor 8X na 8X Max.

Mfululizo wa simu za Huawei Honor umekuwa ni wa kuvutia ambapo mpaka sasa wamefika toleo la nane na kwa ujumla ni rununu za kiwango cha kuvutia halafu kwa bei ya kuvutia.

Kipengele

Honor 8X

Honor 8X Max

Kioo Kioo kina urefu wa inchi 6.5  Full-HD+ (2340 x 1080 pixels) Kioo kina urefu wa inchi 7.12 Full HD+ (1080 x 2244 pixels)
Muonekamo Ina umbo la herufi “V” na mfuniko wa chuma Ina kama mfuniko wa ngozi kwa nyuma lakini si ngozi. Pia, ina “V” mithiri ya tone la maji
Kipuri mama Kirin 710 na Adreno 509 ubora wa ung’avu Qualcomm Snapdragon 636 na kasi yake ni 1.8GHz na Adreno 509 ubora wa ung’avu
Honor 8X na 8X Max

Rununu Honor 8X na 8X Max kwa pamoja.

Kipengele

Honor 8X

Honor 8X Max

Kamera Nyuma: Kamera mbili-MP 20 na MP 2 ambazo zote zina teknolojia ya AI; ukiruhusu AI itaamua ni aina gani ya picha ipige na kwa picha za usiku ina uwezo wa kuunganisha picha nyingi zilizochukuliwa wakati huohuo kuwa kitu kimoja.

Mbele: Ina kamera moja yenye MP 16

Nyuma: Kamera mbili-MP 16 na MP 2.

 

 

 

 

Mbele: Kamera moja yenye MP 8.

RAM/Diski uhifadhi
 • 4GB RAM kwa GB 64 memori ya ndani na
 • 6 GB RAM, 64/128GB memori ya ndani
 • 4GB RAM kwa 64/128GB memori ya ndani
 • 6GB RAM kwa GB 64 memori ya ndani na
Betri
 • 3750 mAh ndio nguvu ya betri na haliwezi kutoka
 • Pia ikiwa na teknolojia ya kuchaji haraka
 • 5000mAh ndio nguvu ya betri na haliwezi kutoka
 • Pia ikiwa na teknolojia ya kuchaji haraka
Honor 8X na 8X Max

Ubora wa picha kwenye kamera ya Huawei Honor 8X.

Kipengele

Pixel 3

Pixel 3 XL

Bei

$205|Tsh. 471,500 (64GB), $305|Tsh. 701,500 (128GB)

$289|Tsh. 664,700 (64GB), $389|Tsh. 894,700 (128GB)

Rangi

Nyeusi, Bluu na Nyekundu

Nyeusi, Bluu na Nyekundu

Mengineyo

 • Inatumia kadi mbili za simu kiwango cha GSM / CDMA / HSPA / LTE,
 • Ina Android 8.1 (masasisho ya Android 9 Pie ni mpaka hapo baadae),
 • ina uwezo wa kukubali memori ya ziada mpka GB 256,
 • Ina sehemu ya kuchoka spika za masikioni,
 • Ulinzi wa kutumia alama ya kidole upo kwa nyuma.
 • Inatumia kadi mbili za simu kiwango cha GSM / CDMA / HSPA / LTE
 • Ina Android 8.1 (masasisho ya Android 9 Pie ni mpaka hapo baadae),
 • ina uwezo wa kukubali memori ya ziada mpka GB 256,
 • Ina sehemu ya kuchoka spika za masikioni,
 • Ulinzi wa kutumia alama ya kidole upo kwa nyuma.
INAYOHUSIANA  Skendo: Samsung Fold zaharibika baada ya utumiaji wa muda mfupi

Honor 8X na 8X Max kuingia sokoni ni mpaka mwezi Oktoba katikati na zinategemewa kuvutia wengi kutokana na sifa zake lakini bei ambayo ni stahimilivu (sio ghali).

Vyanzo: CNET, GSMArena, Gadgets 360, Gizmo China

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.