Kuna kitu kinaitwa YouTube TV ambapo wengi wetu tunaweza tusiwe tunakifahamu lakini kimekuwepo kwa miaka kadhaa sasa na kimekuwa kikifanyiwa maboresho ya hapa na pale ili kukifanya kivutie zaidi.
Kwa zaidi ya miaka mitano sasa YouTube TV imekuwepo kwenye ushindani na ikipatikana kwenye runinga janja halikadhalika rununu (iOS/Android). Si ajabu wasomaji wetu wakisema hawafahamu YouTube TV na kama ni hivyo basi fahamu leo kuwa hii ni huduma inayoonyesha vipindi mubashara kupitia YouTube.
Sasa kwa wale ambao wanaweza kuperuzi kwenye YouTube TV habari njema kwa wanaotumia iOS 15 kuwa programu tumishi husika imeboreshwa kwa kuongezewa kipengele cha Picture-in-Picture kwa maana ya kwamba mtumiaji kuwa na uwezo wa kuangalia vipindi mubashara huku akiwa anafanya vitu vingine kwenye iPhone/iPad.
Uwezo wa kuangalia vipindi huku unafanya vitu vingine inapatikana kwa wateja waliolipia (Premium) kwa Android na iOS. Google haijaweka wazi iwapo itapeleka kipengele hicho kwa watumiaji wote nchini Marekani.
TeknoKona tupo nanyi kila siku na tunazidi kukua kwani sasa tuna programu tumishi kwa upande wa Android ambapo utaweza kupata huduma mbalimbali tofauti na kusoma makala zetu.
Vyanzo: GSMArena, mitandao mbalimbali
No Comment! Be the first one.