fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Google YouTube YouTube Shorts

YouTube Shorts Kuanza Kupatikana Dunia Nzima!

YouTube Shorts Kuanza Kupatikana Dunia Nzima!

Spread the love

Huduma ya YouTube Shorts ni huduma ya video fupi fupi kutoka katika mtandao wa Youtube na huduma hii kwa kiasi kikubwa inafanya kazi kama vile ile ya TikTok.

Kabla ya dunia nzima huduma ilikua inapatiakana kupitia nchi 26 tuu na kwa mara ya kwanza kabisa ilianza kupatikana nchini India.

YouTube Shorts

YouTube Shorts

Ijulikane kwamba hii ni kwa ajili ya video fupi tuu na imewekwa kwa makusudi kuwa changamoto kwa mitandao kama vile TikTok huku Youtube ile ambayo tumeizoea ikiwa inajitegemea.

Kumbuka na TikTok haijalala bado inafanya maboresho mengi kumbuka juzi juzi iliongeza ukubwa wa video zake mpaka dakika tatu.

Soma Zaidi Kuhusu TikTok Ya Dk 3 –> HAPA <–

Muonekano Wa Youtube Shorts

Muonekano Wa Youtube Shorts

Kingine cha msingi ni kwamba TikTok na yenyewe inakuwa kwa haraka sana(pengine kuliko mtandao wa kijamii wowote) na kwa hali hii tuu inabidi YouTube Shorts ijipange sana.

SOMA PIA  Google warahisisha upatikanaji wa taarifa za COVID-19

Ningependa Kusikia Kutoka Kwako, Unadhani Kwa Soko La Sasa YouTube Shorts Inaweza Ikaliteka Soko Na Kuwa Juu Kama Vile Ulivyo Mtandao Wa TikTok?

Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Wa TeknoKona Kila Siku Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania