Kisanayansi, imegundulika kwamba kufanya vitu vingi kwa wakati mmoja hupunguza ufanisi wa kazi. Hatahivyo, mara kadhaa tunajikuta tunahitaji kufanya vitu viwili kwa wakati mmoja.
Kwa mfano, kuna wakati tunahitaji kuangalia video ya maelezo mtandaoni tungali tunafanya kitu husika kwenye kompyuta moja. Zipo njia kadhaa za kufanya hivi.
Kivinjari cha Opera Browser.
Opera Browser toleo jipya kabisa la Windows lina uwezo wa moja kwa moja kucheza video zozote kwenye ki-dirisha Kinachoelea. Unapofungua ukurasa wowote wenye video, kivinjari hiki hukuonesha alama ya kufungua kidirisha cha kuelea amabacho hukaa juu ya dirisha lolote kwenye kompyuta yako kukuruhusu kufanya kazi zako nyingine.
Unaweza kubadili saizi ya kidirisha hiki, kusimamisha video na hata kupeleka video nyuma na mbele. Ukimaliza, unaweza pia kufunga video.
Tumia Visaidizi.
Visaidizi vya vivinjari huongeza uwezo wa kivinjari. Google Chrome na Mozilla Firefox ni vivinjari maarufu na zote zina visaidizi ambavyo husaidia kwa namna moja au nyingine kupata video, hasa za youtube kwenye kidirisha kinachoelea.
Jaribu kupakua visaidizi kadhaa kutoka kwenye google ‘webstore’ au Firefox ‘add-on market’, masoko ya visaidizi hivi na chagua kinachokufaa. Kwa Chrome, jaribu hasa kisaidizi kinachoitwa Floating for Youtube(TM) na kwenye Firefox jaribu Youtube Video Pop-Out.
Tumia Dirisha la Mfumo-endeshaji

Njia ya mwisho na ya moja-kwa-moja ni kwa kufungua dirisha la pekee kwa video yako, iwe ni Youtube au VLC au video kwenye programu nyingine na ilazimishe kukaa juu ya madirisha ya programu nyingine ulizofungua.