Youtube Go inaagwa rasmi, maana mpaka kufikia mwezi wa nane mwaka huu (2022) kampuni itakua ishaachana na huduma hiyo.
Kumbuka hii sio huduma ya kwanza kutoka Google (ALPHABET) kuanzishwa na kuachwa katika kati, nadhani unakumbuka huduma ya Google Plus (Google +) na yenyewe ilianza na baadae ikaenda zake!
Kumbuka pai Youtube Go ni App ambayo ni mbadala ya Youtube ya kawaida ambayo tumeizoea, uzuri wake ni kwamba mtandao huu hauli data (internet) sana.
Hii ni kwa sababu Youtube Go kazi yake kubwa ni kwa ajili ya simu janja za hadhi ya chini na vifaa ambavyo havina uwezo wa internet mkubwa hii ni kwa sababu mtandoa huu unaonyesha mafaili yenye ujazo mdogo kulingnaisha na mtandao wa Youtube tuliouzoea.
Mpaka sasa YouTube Go imetimiza miaka sita tangia kuanzishwa kwake na imekua msaada mkubwa kwa wale ambao wana matumizi madogo ya data (internet) katika vifaa vyao.
Ukiachana na Mtandao huu kwa nyota yake kufa, kumbuka kama ulikua ni mtumiaji unaweza kurudi na kuendelea kutumia YouTube ile ambayo tumeizoea.
Ningependa kusikia kutoka kwako, hili wewe unalipokeaje? je unaona sio sawa kwa mtandao huo kuruhusiwa kufa? niandikie hapo chini katika uwanja wa comment.
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.