Samsung wametambulisha rasmi matoleo yajayo ya familia ya simu zake maarufu zinazotumia jina la Galaxy S. Kupitia makala hii pata kuzifahamu kwa undani simu mpya za Samsung Galaxy S7 na S7 Edge.

Samsung Galaxy S7: Kipi ni cha kipekee?
Ingawa kwa haraka haraka inaweza ikaonekana kimuonekana matoleo ya Samsung Galaxy S7 na S7 Edge yanafanana na yale ya S6 na S6 Edge ukweli ni kuwa kuna maboresho makubwa yamefanyika kwa ndani.
Kuna vitu kadhaa ni vipya na vingine vingi vimeboreshwa zaidi.
Samsung Galaxy S7: Sifa za undani

Tofauti kuu ni uwepo wa kioo kilichopinda pembeni mwake katika S7 Edge ambacho kinaonesha ‘notifications’, habari na matumizi mengine. Samsung Galaxy S7 Edge inakuja na inchi 5.5 wakati Galaxy S7 inakioo cha inchi 5.1 na pia zikiwa na ‘resolution’ ya pixels sawa, 2560×1440
-
Ni nyembamba kuliko toleo la S6, Galaxy S7 na S7 Edge zinaupana wa mm 7.9.
-
Kioo (display) cha inchi 5.1,Quad HD AMOLED
Kuna teknolojia ya ‘Always-on Display’ imetumika. Teknolojia hii ambayo ilitumiwa kwanza na LG katika simu yake ya LG G5 inaruhusu sehemu flani tuu ya kwenye kioo cha simu kutozika pale simu inapozima mwanga wa kioo.
Kupitia sehemu hii utaweza kuendelea kuona ‘notification’ muhimu kama vile muda, tarehe n.k – haya yote bila ku-unlock simu yako.
Pia wanasema display hii itatumia chaji kidogo zaidi ukilinganisha na kwenye S6
-
Kiwango cha RAM cha GB 4 pamoja na prosesa ya Snapdragon 820 na zingine zitakuwa na prosesa ya Exynos 8890
-
Kiwango cha diski uhifadhi cha GB 32 au GB 64 huku wakiwa wamerudisha uwezo wa kutumia memori kadi (microSD)
-
Inakuja na kamera ya Megapixel 12 (f/1.7)
Kamera katika Galaxy S6 ilikuwa megapixel 16, ingawa zimepunguzwa katika Galaxy S7 ila imetokea kutokana na maboresho mengine ya kamera yaliyofanyika hasa hasa katika kuongeza uwezo na ubora wa picha katika maeneo ya mwanga mdogo.
Kuna teknolojia ya ‘Dual pixels’ iliyotumika inayosaidia kufanya picha ziweze kupigwa kwa haraka zaidi bila kuathiri ubora wake.
Kamera ya selfi ni ya Megapixel 5
-
Betri ya mAh 3000 kwa Galaxy S7 na huku Galaxy S7 Edge ikiwa na mAh 3600
Uwezo wa kuchaji bila utumiaji wa waya (Wireless charging)
-
Pia zina uwezo wa kutopitisha maji na kutoharibiwa kirahisi na uchafu (Kimombo: water & dust resistance)
-
Pia zinakuja na toleo la kisasa kabisa la Android 6.0.1 Marshmallow likiwa na muonekano wa TouchWiz
Upatikanaji
Zinategemewa kuanza kuingia sokoni kuanzia mwezi wa tatu tarehe 11. Zinakuja katika rangi Nyeusi, Nyeupe, Dhahabu na ‘silver. Bei bado hazijawekwa wazi.
Je, una maoni gani juu ya ujio huu wa Samsung Galaxy S7 na S7 Edge?
One Comment
Comments are closed.
[…] toleo jipya kabisa la iOS 9. Inategemewa ujio wa simu mpya za kisasa zaidi kwa mwaka huu kama Samsung Galaxy S7 n.k zitasaidia kukuza asilimia ya watumiaji wa Android Marshmallow […]