Makampuni mengi yamekuwa kazini wakiboresha muda ambao simu janja inatumia kujaa chaji na yamekuwepo mabadiliko mengi kwa miaka kadhaa sasa. Xiaomi wamekuwa na kiu ya kuboresha teknolojia ya kuchaji haraka.
Xiaomi imekuwa katika ushindani na kampuni nguli kwenye ulingo wa biashara ya simu janja na kampuni hiyo imekuwa ikishika nafasi za juu mara kwa mara kulingana na tathimini inayofanywa na mashirika mbalimbali. Kwenye suala zima la teknolojia ya kuchaji haraka Xiaomi wamekuwa hodari wa kufanya maboresho na kuzidi kwenda juu.
Ilikuwa ni habari za chini kwa chini lakini sasa inawezekana kuwa ni kweli kwani zipo taarifaa kuaminika kuwa Xiaomi inafanya majaribio ya teknolojia ya kuchaji haraka kwa 150W. Xiaomi wanafahamika vilivyo kwenye mapambano haya ya kuwa na simu janja ambayo inajaa chaji ndani ya muda mfupi sana.
Wakati fulani huko nyuma Xiaomi walitoa simu janja ambayo inaweza kukubali kuchajiwa kwa teknolojia ya haraka 120W na sasa wanaona wakati umefika wa kutoa kitu bora zaidi; hapa nazungumzia 150W. Unafikiri rununu itakayokuwa na teknolojia hiyo inaweza kuchukua dakika ngapi kujaa chaji?
Xiaomi Mi 10 Ultra ni simu janja ambayo ina teknolojia ya kuchaji haraka kwa nguvu ya 120W.
Je, ni simu janja gani itakuwa na uwezo wa kuchaji haraka kwa 150W?
Inaaminika kuwa Xiaomi Mix 5 ambayo inaelezwa kuwa na teknolojia za kuvutia basi ndio simu janja ambayo itakuwa na uwezo wa kujaa chaji kwa nguvu ya 150W. Kuhusu lini itatoka hilo bado halijafahamika.
Hiyo ndio vita ya kutaka kuwa na kifaa cha kidijiti ambacho kinachukua dakika kadhaa tuu kujaa chaji na mtu akaendelea kutumia simu janja yake. Je, simu unayotumia inachukua muda gani kukaa kwenye chaji hadi kujaa? Tuambie.
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
No Comment! Be the first one.