Katika ulimwengu wa sasa simu janja ambayo inakuwa na kasi zaidi inayokea kujizolea sifa kwani ufanisi wake unakuwa umezidi rununu nyingine kwa nyanja mbalimbali. Xiaomi 12 inatajwa kuja kuwa simu janja yenye kasi zaidi duniani. Je, unafahamu sababu?
Inaposemwa kuwa simu janja kuwa na kasi kubwa moja kwa moja hapa kiini chake ni kipuri mama ambacho kilichowekwa kwenye rununu husika. Qualcomm ni kampuni ambayo imejikita zaidi kwenye utengenezaji wa vipuri mama ambavyo vinatumika kwenye simu janja za makampuni mbalimbali kama Samsung, Xiaomi na mengineyo.
Hivi karibuni Qualcomm wamefanya maonyesho ya kwao ya teknolojia ambapo wametangaza kipuri mama Snapdragon 8 Gen 1 ambacho kinaelezwa kuwekwa kwenye simu janja kadhaa ikiwemo Xiaomi 12 na kuelezwa kuwa ndio itakuwa rununu yenye kasi zaidi duniani.
/cdn.vox-cdn.com/uploads/chorus_image/image/70212207/Snapdragon_8_Gen_1_Mobile_Platform__Key_Visual__Angle_2.0.jpg)
Machache kuhusu Xiaomi 12 na Qualcomm Snapdragon 8 Gen 1
Kipuri mama tajwa kinakuja na teknolojia ya 5G hivyo Xiaomi 12 na hata nyinginezo ambazo zitakuwa na kifaa hicho nazo pia zitakuwa ni za 5G. Ujio wa simu janja hii haujawekwa wazi lakini kwa habari zilizopo chini ya kapeti ni kwamba rununu hii itazinduliwa Disemba 12.
Simu janaja nyingine ambayo ina kipuri mama tajwa ni Realme GT 2 Pro, Motorola Edge X30 halikadhalika Oppo, OnePlus, iQOO wamethibisha simu janja zao zijazo zitakuwa na kipuri mama kipya chenye nguvu na kasi zaidi duniani.
Vyanzo: GSMArena, mitandao mbalimbali
No Comment! Be the first one.