fbpx

Google Imechoshwa Na Wizi Wa Baiskeli Zake!

0

Sambaza

kampuni nguli katika maswala ya teknolojia kwa ujumla, Google imechoshwa na vitendo vya wizi wa baiskeli zake

Google katika eneo lake ina baiskeli zaidi ya 1,100 na kila wiki zinaibiwa baiskeli katika ya 100 -250. Baiskeli hizi ni spesheli kwa ajili ya wafanya kazi wake.

Baiskeli Kutoka Google

Ni kwamba wafanya kazi wanazitumia hizi kuzunguka zunguka ndani ya eneo la ofisi, na pia hii imekua ni njia bora ya kusaidia watu(wafanyakazi) kuendana na muda.

Baiskeli hizi zimepigwa rangi nzuri ambayo inaendana na zile ambazo zipo katika logo ya Google.

Baiskeli hizi ilibidi zitumike na wafanyakazi tuu lakini cha kushangaza ni kwamba wakazi ambao pia ni majirani inasemekana huwa wanaziiba baiskeli hizo mara kwa mara.

Baiskeli Kutoka Google

Baiskeli hizi zimekuwa zikionekana katika viwanja mbali mbali katika makazi ya watu, katika kumbi za michezo na cha ajabu ni kwamba hata kwenye tangazo la bidhaa za Garnier baiskeli hizi zilionekana.

INAYOHUSIANA  Verily, kuja na viatu vyenye uwezo wa kumpima mvaaji uzito

Kampuni ilimua kuweka mfumo wa GPS katika baiskeli hizo mwaka jana, na baada ya hapo ikagundulika kuwa baiskeli hizo zinaenda mbali sana kama vile Mexico, Nevada na maeneo mengine.

Bado juhudi zingine nyingi tuu zinafanywa na kampuni ili kuhakikisha kuwa baiskeli zake zinakuwa salama kwa wafanya kazi wake tuu.

Ningependa kusikia kutoka kwako, hii  umeipokeaje? niandikie hapo chini sehemu ya comment? je una baiskeli? je ipo salama? (hahaha!)

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.