fbpx
Kompyuta, Microsoft, Teknolojia

Windows 98 yatimiza miaka 20 tangu kuzinduliwa kwake

windows-98-yatimiza-miaka-20-tangu-kuzinduliwa-kwake
Sambaza

Miaka ishirini iliyopita Window 98 ilizinduliwa rasmi ulimwenguni. Wakati huo Microsoft ilikuwa kampuni tofauti na Bw. Bill Gates alikuwa Mkurugenzi Mtendaji.

Windows 98 ilizinduliwa Juni, 25 1998 na kupatikana katika nchi zaidi ya 40 ulimwenguni kote na kuuzwa katika maduka ya rejereja zaidi ya 12,000 nchini Marekani.

Windows 98 ilitolewa baada ya Windows 95 ambayo ilitolewa miaka mitatu nyuma na kufanya mabadiliko makubwa na mapinduzi ya mfumo endeshi katika Kompyuta duniani. Mabadiliko hayo ilikuwa na kuja na mfumo wa 32-bit, Start menu, Taskbar, n.k.

INAYOHUSIANA  Uhalifu mtandao: Makosa ya mtandaoni yaliyoripotiwa kwa mwaka 2017
miaka 20 tangu kuzinduliwa
Windows 98 ilikuja na mengi ya kuishi mpaka sasa na kuleta mabadiliko ya kusafisha na kuheshimu Windows 95 kwa kuongeza ubora zaidi katika jukwaa la Microsoft.

Ikiwa imetimiza miaka 20 Windows 98 ilikuwa na mfumo wa endeshi imara pia iliboresha kwenye usanifu wa vifaa ikiwemo kuruhusu matumizi ya USB na kufungua ulimwengu mpya wa watumiaji wa kompyuta.

Katika kuimarisha na kurekebisha kasoro za Windows 98 baadae walitoa toleo la Windows 98 SE kama toleo la pili la Windows 98.

Baada ya Windows 98, ilifuatiwa na matoleo ya Windows 2000 (17 Feb 2000), Windows ME (14 Septemba 2000), Windows XP (25 Okt 2001), Windows Vista (25 Aprili 2005), Windows 7 (22 Julai 2009), Windows 8 (26 Okt 2012) na Windows 10 (29 Juai 2015).

Kuna haja ya kuikumbuka Windows 98 kwa mengi mazuri japo imefutwa na ujio wa matoleo mengnei ya programu endeshi (Windows) zilizokuja na mabadiliko makubwa zaidi na ya kisasa lakini misingi yake ilianzia kwa Windows 98.

INAYOHUSIANA  Takwimu za Tanzania na uhalifu wa kwenye mtandao #Uchambuzi #Ripoti

Wakati tukiadhimisha miaka 20 ya Windows 98 je, wewe uliwahi kutumia Windows 98? Au kuiona Kompyuta iliyo na Windows 98?

Facebook Comments

Sambaza
1 Comments
Share

Siyan

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

1 Comments

  1. Windows 98 yatimiza miaka 20 tangu kuzinduliwa kwake – TeknoKona Teknolojia Tanzania
    June 28, 2018 at 1:06 pm

    […] post Windows 98 yatimiza miaka 20 tangu kuzinduliwa kwake appeared first on TeknoKona Teknolojia […]