fbpx
Kompyuta, Windows, Windows 10

Windows 10 : Sasa chomoa kifaa cha USB Drive/Flash bila kufuata utaratibu

window-10-kuchomoa-kifaa-cha-usb-drive

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163
Sambaza

Microsoft katika toleo la kisasa la Window 10 (kuanzia toleo la Oktoba 2018) imewezesha watumiaji wake kuweza kuchomoa kifaa cha USB Flash/Drive kwa usalama bila kufuata hatua ya ‘Safely Remove’.

Microsoft wamesema katika ukurasa wao wa habari kuwa  kwa kipindi kirefu kuna machaguo ya aina mbili ya kuchomoa vifaa vya USB kwenye eneo la mipangilio/Setting. Kuna sera/uwezo wa Quick removal na Better performance. Zamani mpangilio wa ‘Better Performance‘ ndio ulikuwa mpangilio mkuu ila sasa inakuwa Quick Removal.

  • Quick removalsera hii itakuwa ya mwanzo kabisa ambayo itawezesha kuchomoa kifaa ya diski uhifadhi cha USB (flash) yako muda wote bila kufanya chochote
  • Better performance –sera hii ni nzuri na inaongeza ufanisi na mawasiliano ya kidata kati ya kompyuta na kifaa cha USB Drive/flash. Pia njia hii inahakikisha data zako zinakuwa salama zaidi dhidi ya kuharibika kama wakati imechomolewa kulikuwa na usafirishaji data kati ya kompyuta na kifaa chako cha USB. Lakini endapo mtumiaji akichagua basi itamlazimu kutumia shortcut ya Safe Removely kabla ya mtu kuchomoa kifaa cha usb flash.
INAYOHUSIANA  Xiaomi wawatania Apple kwa kuuza bidhaa kwa mafungu kwa majina ya XR, XS na XS Max

picha : microsoft

Sehemu ya kuchagua policy mpya ya kutolea USB FLASH kwenye window

JINSI YA KUWEZESHA SERA HIZI:

  • Bonyeza Right Click sehemu ya My Computer/ This Pc alafu chagua Manage

kuchomoa kifaa cha usb

  • Alafu chagua Disk Management

  • Alafu kwenye sehemu ya usb flash yako (eg, disk *) right click then chagua Properties

  • Baada ya hapo sasa unaweza chagua/badalisha chaguzi unayoitaji

kuchomoa kifaa cha usb

MUHIMU : kama unajali kuhusu usb flash yako basi vyema tu kuweka Better Performance

INAYOHUSIANA  Mwisho Wa Google Kusasisha (update) Chrome Inayotumika Kwenye Windows XP Waja!

JE, wewe ungependa kutoa USB FLASH yako bila kufanya chochote? Kwa kiasi kikubwa Microsoft wamewezesha hili kwa sababu tayari tabia za watumiaji wengi wa kompyuta ni wanaochomoa tuu bila kufuata utaratibu wa ‘Safely Remove’.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Lymo

A Cyber Security Guy | A student | I Know A lot