Biashara ya mtandaoni imeweza kurahisisha upatikanaji wa vitu na hivyo kuokoa vitu mbalimbali kama vile muda na gharama kutokana na urahisi wa upatikaji wa bidhaa husika. Watanzania hasa wanaoishi jiji kuu la biashara, Dar wanatarajia kufurahia wiki moja ya kununua vitu kwa bei nafuu mtandaoni.
Iwapo wewe ni wale ambao umekuwa mtumiaji mzuri wa tovuti ambazo zinafanya biashara mtandaoni basi unafahamu fika kuwa kuna siku kadhaa kampuni hisika inaamua kushusha bei ya bidhaa za vitu fulani fulani katika kipindi cha wiki moja au zaidi kulingana na ambavyo wahusika wamepanga.
Kwa kawaida ikifika kipindi ambacho kuna punguzo la bei kwa bidhaa tunasema “Black Friday” lakini ya mwezi huu wa Aprili 2019 naomba niite “Black Monday” kwa sababu kuanzia Aprili 8-14 2019 (usiku wa Jumatatu) kuanzia saa sita kamili USIKU juu ya alama Jumia Tanzania watauza vitu kwa punguzo katika kipindi cha wiki moja.

Sitaki nielezee namna ya kufanya manunuzi kupitia Jumia Jumia Tanzania kwani ukitembelea tovuti/programu tumishi yao tu utaweza kujua ni jinsi gani ilivyo rahisi kujihakikishia kuwa umeshafanikiwa kuweka ombi la kununua bidhaa fulani LAKINI kama ukiwa mjanja zaidi na mfuatiliaji wa karibu kabisa wiki ya bei nafuu kwa bidhaa za kidijiti unaweza kujikuta unanunua simu janja MPYA kwa bei rahisi SANA.

TeknoKona tumeweza kuwaletea habari njema watu wote ambao kununua kitu mtandaoni sio kitu cha kuogofya bali unafanya malipo ukisubiri mzigo kwa muda ambao utaarifiwa ukaufuate au mahali ambapo utachagua wakuletee.
Chanzo: Jumia Tanzania