fbpx
Android, apps, iOS, simu, whatsapp

WhatsApp yaleta kipengele kipya kwenye makundi #Masasisho

whatsapp-yaleta-kipengele-kipya-kwenye-makundi-masasisho
Sambaza

WhatsApp isiyoishiwa na vitu vipya kila mara kwani ni siku chache tu zimepita na tayari imewezesha mtu kujua mahali ulipo kwa njia ya kusambaza na kama hiyo haikutosha basi imeleta kipengele kingine ambacho kinaweza kabisa kusumbua kwenye makundi ya kwenye WhatsApp.

Kutokana na taarifa rasmi imeelezwa kuwa katika sasisho lijalo kwenye WhatsApp basi kama wewe upo kwenye kundi lolote kwenye WhatsApp utaweza kupiga simu aidha ya sauti au video kwa wana kundi wote na kuweza kuwasiliana kwa wakati mmoja. Eeh! Si itakuwa poa hiyo? 😆  😆

INAYOHUSIANA  WhatsApp Business yaanza kupatikana; Sasa unaweza ukafungua akaunti ya kibiashara

Sasisho la kuweza kupiga simu za sauti/video litaanza kupatikana kwa wanaotumia WhatsApp Beta toleo la 2.17.70 (Android/iOS).

Kwa njia ya kupiga simu kwenye kundi mnaweza kusikilizana wote cha msingi ni kifurushi cha kutosha cha intaneti.

Mengineyo yaliyofichwa kwenye sasisho litakalotoka hivi karibuni kwenye WhatsApp Beta.

Toleo la WhatsApp 2.17.70 kutuma ombi kwenye server kuuliza kama yule unayempgia anawasiliana kwa njia ya sauti/video kwenye kundi lingine.

Kuwataarifu watu wote ambao umehifadhi namba zao kwenye simu yako pale unaapobadilisha namba unayotumia kwenye WhatsApp. Hii inamaanisha mara tu unapobadilisha namba kwenye WhatsaApp, watu wote kwenye simu yako watapata taarifa fupi kuwa umebadilisha namba ya kwenye WhatsApp.

Kusitisha kile ulichotuma kwa marafiki, kwa kimombo tunasema ‘Delete for everyone’ ikimaanisha kuwa utakuwa una uwezo wa kufuta kile ambacho umekituma aidha kimakosa au hutaki tena ujumbe ule uwafikie. Utawza kufuta iwe sms au picha/video au GIFs ulizosambaza ndani ya dakika tano.

Masasisho hayo yanaweza kuanza kupatikana kwa watumiaji wote wa WhatsApp ndani ya wiki kadhaa zijazo ingawa hapo awali ilifahamiks kuwa masasisho hayo huwenda yakaanza kupatikana mapema mwakani.

Cha kufanya sasa ni kutumia WhatsApp Beta na kujua zaidi kuhusu toleo la Beta kwenye WhatsApp BOFYA HAPA!. Tuambie, umeipokeaje habari hii?

Vyanzo: IndiaTodaayinTech, IndependentUK

Facebook Comments

Sambaza
1 Comments
Share

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

1 Comments

  1. Kufuta Meseji WhatsApp: Sasa ni rasmi kwa watumiaji wa app hii maarufu
    November 2, 2017 at 5:47 pm

    […] ya kiu ya watumiaji wa WhatsApp kusubiri kipengele cha kuweza kufuta meseji uliyomtumia mtu, sasa rasmi kipengele hicho kimewezeshwa kwa watumiaji takribani wote duniani […]