fbpx
apps, whatsapp

WhatsApp waja na aina mpya ya Muandiko (font style)

whatsapp-waja-na-aina-mpya-ya-herufi-font-style
Sambaza

Je haupendi aina ya mwandiko uliopo katika app ya WhatsApp? Usihofu, WhatsApp wapo njiani kuleta aina mpya ya muonekano wa herufi zake (font style) na muda wowote kuanzia sasa utaweza kuzitumia.

Maboresho haya yameshaonekana katika matoleo ya WhatsApp yaliyo katika matengenezo, yaani ‘Beta’.

WhatsApp waja
Aina mbalimbali za mionekano ya herufi inayowezekana katika WhatsApp kwa sasa, mwishoni ndio muonekano wa ‘font’ mpya

Aina ya font utakayoweza tumia inafahamika kwa jina la FixedSys na unaiweza kuiona kupitia kompyuta yako ya Windows au ata kwa kutafuta Google.

INAYOHUSIANA  Jinsi ya kujitoa au kutoa namba yako kutoka kwenye app ya TrueCaller (2019)

Tatizo kuu ni jinsi ya kuitumia, inaonekana kama WhatsApp hawatatafuta njia rahisi kabisa ya font hiyo kutumika basi inawezekana wengi wakaona ni kazi kweli kuitumia mara kwa mara. Kuweza kutuma ujumbe katika muonekano huo inabidi unapoandika uweke alama tatu za kufungua na kufunga semi – mwanzoni na mwishoni…yaani ‘. Mfano – ”’UJUMBE WAKO”’

Kwa sasa uwezo huo upo katika toleo la beta, toleo namba  2.16.179 kwa Android na pia ata kwa iOS tayari lishaanza lishaanza kuonekana kwa watumiaji wa WhatsApp beta.

INAYOHUSIANA  AmpMe: App Inayogeuza Simu Janja Kadhaa kuwa Spika Zikipiga Wimbo Mmoja

Ukiacha hili pia inasemekana WhatsApp wapo njiani kuleta uwezo wa kutumia video fupi za mfumo wa GIF na pia uwezo wa kupiga na kupokea simu katika mfumo wa video.

Soma Pia

INAYOHUSIANA  Periscope sasa kuruhusu video kukaa muda mrefu! #Apps

Endelea kutembelea mtandao wako wa TeknoKona kwa habari na maujanja mbalimbali ya Teknolojia!

Vyanzo: Na mitandao mbalimbali

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share
Tags: ,

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |