fbpx
apps, Facebook, Intaneti, whatsapp

WhatsApp kutuma data zako kwenda mtandao wa Facebook!

whatsapp-kutuma-data-zako-kwenda-facebook

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163
Sambaza

WhatsApp walikuwa wanakipinga kwa muda mrefu sana suala la huduma zinazotumia data kuhusu watumiaji wake kimatangazo n.k, lakini miaka kadhaa baada ya kununuliwa na Facebook inaonekana hilo linabadilika.

whatsapp facebook whatsapp kutuma data

Katika taarifa iliyotolewa katika blog yao WhatsApp wametangaza rasmi mwanzo wa utaratibu wa app yao kutuma data mbalimbali kwenda huduma ya Facebook ambapo data hizo zitatumika kwa mambo mbalimbali hii ikiwa ni pamoja na matangazo.

INAYOHUSIANA  Jinsi ya kuficha au kufichua mazungumzo kwenye WhatsApp

Wengi walioona suala la data kuhusu watumiaji wa WhatsApp kuwa sababu kubwa kabisa ya Facebook kulipa mabilioni kununua huduma ya WhatsApp.

Baadhi ya data ambazo zitakuwa zinatumwa kwenye mitambo ya Facebook ni pamoja na namba za simu za watumiaji wa huduma ya WhatsApp na inasemekana matumizi ya data hizi ni pamoja na kuboresha mfumo wa marafiki wa Facebook (Friends Recommendations) na pia mfumo wa matangazo.

INAYOHUSIANA  TikTok: App iliyokuwa kwa kasi mwaka 2019, tishio kwa Facebook

Wengi wanaona kitu kikubwa zaidi kinachoitajiwa na Facebook ni data za watumiaji wa app hiyo ambazo zinaweza tumika kuboresha matangazo ya mtandao huo, na hapa ndio wengi wanaona kutakuwa na matumizi mabaya ya data za watumiaji wa app hii maarufu.

Huduma shindani kwa WhatsApp ya kuchati ya app ya Telegram inaonekana ndio huduma pekee kwa sasa ambayo watumiaji ambao hawatapendezwa na suala la data zao kutumiwa na mtandao wa Facebook wanaweza kuamia.

INAYOHUSIANA  Kiswahili kutumika katika Microsoft Translator

Tuambie, je wewe unajali sana suala la usalama na usiri (privacy) wa data zako kwenye huduma za kimtandao na apps? Au unaona kwa kuwa unafurahia huduma basi wawe na uhuru wa kutumia data zako?

Vyanzo: TheVerge na mitandao mbalimbali

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |