fbpx

WhatsApp kutotuma data za watumiaji wake kwenda Facebook. #Uingereza

0

Sambaza

WhatsApp kutotuma data za watumiaji wake kwenda Facebook kwa sasa ni kitu cha uhakika kwa watumiaji wa baadhi ya nchi.

Uwamuzi wa Facebook kununua app hii maarufu mwaka 2014 ulichukuliwa na wengi kuwa lengo kuu ni kwa Facebook kuona jinsi ya kutumia data zinazowahusu mamilioni ya watumiaji.

WhatsApp kutotuma data za watumiaji wake kwenda Facebook

Na kuna kipindi kulifanyika mabadiliko machache kwenye app hiyo yaliyoonesha mwanzo wa Facebook kutaka kuanza kupata data za watumiaji wa app hiyo – watu wengi walilalamika sana na ndio ikaleta chunguzi nyingi kutoka vyombo vya usalama wa data vya serikali mbalimbali ikiwemo ya Uingereza.

Chombo cha serikali ya Uingereza kinachohusiana na taarifa, ICO – Information Commissioner’s Office, kilifungua uchunguzi kama WhatsApp wanatuma data kuhusu watumiaji wake kwenda tovuti ya Facebook. ICO walidai kufanya hivyo kungekuwa ni uvunjifu wa sheria na mkataba katika ya app ya WhatsApp na mamilioni ya watumiaji wake.

INAYOHUSIANA  Vitu vipya kwenye WhatsApp safari hii

ICO imekuja na matokeo ikisema imejiridhisha kabisa ya kuwa kwa sasa app ya WhatsApp haitumi data za watumiaji wake kwenda kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook.

Ukitoa Uingereza tayari kuna chunguzi za namna hiyo nchini Ufaransa, Ujerumani na Italia. Kuna wasiwasi kama kwa nchi ambazo hazijaweka taratibu za kuwalinda wananchi wake dhidi ya matumizi yasiyo rasmi ya data – kama Facebook wanafuata utaratibu wowote kuhusu kutotumia data za watumiaji.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.