fbpx

Apple, apps, iOS, whatsapp

WhatsApp Business kwenye simu za iPhone

whatsapp-business-kwenye-simu-za-iphone

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Sambaza

Uwepo wa teknolojia umefanya biashara za watu duniani kuweza kuwafikia watu wengi kwa urahisi na vitu vikaweza kufanyika bila ya hata kuonana ana kwa ana. WhatsApp Business ni moja kati ya vitu ambavyo vimerahisisha mawasiliano kati ya mfanyabiashara na wateja wake ingawa si kwa wote bali wale wanaoitumia.

Tangu Septemba 2017 kwenye Android mtu anaweza  akawa anatumia WhatsApp mbili tofauti; moja ile ambayo wengi tunaifahamu na nyingine ikiwa imetengenezwa ikilenga mambo yanayohusu biashara mathalani kuhusu biashara husika, mahali ofisi ilipo, tovuti/anwani ya barua pepe, n.k.

SOMA PIA  WhatsApp ya Android Yapata 'Update': Fahamu Mambo 5 Yaliyoboreshwa

Tangu wakati huo mpaka Aprili 2019 wanaotumia mfumo endeshi wa iOS nikizillenga simu za iPhone nao sasa wataweza kutumia toleo la WhatsApp mahususi kabisa kwa ajili ya kufanya biashara kidijitali zaidi na hivyo kuwa katika nafasi nzuri ya kutenganisha mawasiliano yako na watu wengine na yale yanayohusu biashara pekee.

WhatsApp Business inawezesha mtu kutuma ujumbe wa papo hapo kulingana na alichokiandika, kuweza kuweka ujumbe iwapo umetoka kikazi/utarejea baada ya siku gani.

kwenye simu za iPhone
WhatsApp Business yasogwezwa kwenye simu za iPhone.

Kwa kuanza WhatsApp Business kwenye simu za iPhone zinapatikana kwenye nchi za Brazil, Ujerumani, Indonesia, India, Uingereza, Marekani na Mexico. Kwa nchi zingine itaanza kupatikanakatika siku za usoni (kama bado haijawekwa kulingana na nchi uliyopo). Pia toleo hilo linaweza kutumiwa kupitia kompyuta.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Sambaza

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|