fbpx

WhatsApp: Watumiaji wa GB WhatsApp na WhatsApp Plus hatarini kufungiwa milele

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +

ICT CONFERENCE 2019

Sambaza

Zoezi la WhatsApp kuwafungia kwa muda watumiaji wa GB WhatsApp na WhatsApp Plus lilianza takribani miezi miwili iliyopita limezidi kuchachamaa, na sasa kampuni ya WhatsApp imetoa angalizo kwa wale ambao hurudi tena kwenye apps hizo tena na tena.

watumiaji wa gb whatsapp na whatsapp plus

Je wewe ni mtumiaji wa GB WhatsApp au WhatsApp Plus? Muda wa kuachana nazo ni sasa.

Katika taarifa rasmi iliyotolewa na WhatsApp – inayomilikiwa na kampuni ya Facebook, wamesema “kama unapokea ujumbe ndani ya app ikisema akaunti yako imefungiwa kwa muda (temporarily banned) ina maanisha unatumia toleo lisilo rasmi la WhatsApp.

Kama hautobadili na kuanza kutumia toleo rasmi la WhatsApp baada ya muda ya kufungiwa, akaunti yako ipo katika hatari ya kufungiwa mazima kwenye huduma ya WhatsApp.”

Tayari Facebook wameonesha wapo njiani kukaribisha matangazo kwenye app ya WhatsApp na hivyo uwepo wa matoleo ya WhatsApp ambayo si rasmi ni hatari katika mpango wao huo. Ila pia ni matoleo ambayo data za mtumiaji zipo kwenye hatari ya udukuzi.

INAYOHUSIANA  Programu tumishi kutoka kwa msanii wa Tanzania

watumiaji wa GB Whatsapp na whatsapp plus

Je upo tayari kuhamia toleo rasmi? Basi fuata njia hizi kuhakikisha haupotezi data zako za mazungumzo

Kama ulikuwa unatumia GB WhatsApp:

  • Subiria muda wa kufungiwa kupitia (temporary ban)
  • Kisha ingia kwenye GB WhatsApp na kisha nenda – More Options -> Chats -> Backup Chats
  • Kisha nenda kwenye app ya Files na kisha tafuta faili la GB WhatsApp, ukilipata libadili jina (rename) kutoka GB WhatsApp kwenda jina la WhatsApp
  • Nenda Google PlayStore na shusha app ya WhatsApp, fungua na hakiki namba
  • Itakapokuletea suala la Backup, bofya Restore -> Next
  • App ya WhatsApp itatumia data za chati za GB WhatsApp na sasa utaweza kuiondoa GB WhatsApp.
INAYOHUSIANA  Whatsapp Yapata Muonekano Mpya wa 'Material Design'

Kwa watumiaji wa WhatsApp Plus hali ni tofauti kwani hauitaji kuchukua hatua nyingi. Hakikisha umefanya backup, kisha install app ya WhatsApp. App ya WhatsApp itaweza kurudisha data za WhatsApp Plus moja kwa moja kwenye hatua ya kurestore.

Tunakushauri kama umekuwa mtumiaji wa WhatsApp Plus na GB WhatsApp kama namba unayotumia ni muhimu kwako kwa mawasiliano ni bora uhamie kwenye WhatsApp rasmi.

INAYOHUSIANA  Microsoft Apps : Soko la Apps za Microsoft kwa Ajili ya Simu na Tableti za Android

Bado WhatsApp hawajoa taarifa ya ni mara ngapi itachukua mtu kurudia kutumia matoleo yasiyo rasmi ili namba yake kufungiwa moja kwa moja ila tunaamini wanaweza kuanza kuchukua hatua hii muda wowote kuanzia sasa.

Chanzo: WhatsApp Blog
Facebook Comments

Sambaza

ICT CONFERENCE 2019

Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.