Kumbuka Fitbit ilikamilisha kununuliwa na Google mwaka 2021, lakini bado kampuni hiyo ya utimamu wa mwili na baadhi ya vifaa vya kielektroniki ilikua ikijitegemea kwa kiasi kikubwa.
Kwa sasa Google inataka ijulikane kabisa kuwa iko chini ya Google na mabadiliko kadha wa kadha yanafanyika mpaka kupelekea huduma hii kuwa “Fitbit By Google”
Kinachofanyika ni kwamba kuanzia 2023 watumiaji wote wa huduma za Fitbit na vifaa vyake itabidi wahamie katika akaunti za Google mpaka kufikia 2025.
Kingine ni kwamba huduma hii inaweza kupatikana kabisa katika vifaa vya google moja kwa moja. Kwa sasa kampuni ya Apple kupitia vifaa vyake vya mawasiliano kama vile iPhone….
…. vinavyotumia iOS 16 na kuendelea zinakuja na App kabisa ijulikanayo kama ‘Fitness’ ambayo ni mahususi kwa ajili ya utimamu wa mwili.
Pengine ‘Fitbit By Google’ inaweza kaunza kupatikana katika vifaa vya Google kama vile Google Pixel na vingine vingi kama saa janja kutoka katika kampuni hiyo.
Fitbit wenyewe wamekiria kuwa yote haya yanafanyika (kuanza kuingia kutumia akaunti za google au kuhamia na kuanza kutumia akaunti za google) na yataendana sawa sawa na sera za makampuni yote mawili
Nao Google wamesema kuwa itatofautisha huduma zake nyingi tuu na Fitbit, huduma kama zile za kuonyesha matangazo hazitakau na nafasi ya kuonekana.
watumiaji wataweza kuingia katika akaunti zao kwa kutumia njia za kawaida za ku’log in katika akaunti zao za Fitbit au wanaweza kuingia kwa kutumia kipengele cha “continue with Google.”
Soma Kuhusiana Na FitBit >>HAPA<<
Ningependa kusikia kutoka kwako, naindikie hapo chini katika eneo la comment, je hii umeiopokeaje? Japokuwa inamilikiwa na Google je ilikua na haja ya kufanya yote haya?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
No Comment! Be the first one.