fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

tecno

simu Tanzania Tecno

Tecno kutoa Zawadi kwa Watakaoilipia Tecno Camon 16s mapema. #Preorder

tecno

Kampuni ya Tecno kutoa zawadi kwa watakaoilipia simu ya Tecno Camon 16s mapema, yaani kufanya ‘pre-order. Simu ya Tecno Camon 16s inatarajiwa kuanza kupatikana sokoni hivi karibuni.

Katika taarifa waliyoitoa kama sehemu ya promosheni ya ujio wa simu hiyo, Tecno Tanzania wamesema kwa mteja yeyote atakayefanya malipo mapema ya ununuaji wa simu hiyo kabla ya ujio wake rasmi basi atapata zawado za paopo kwa hapo zitakazohusisha vitu kama vile betri la kuchaji la ziada la Tecno (power bank) na spika ndogo ya mfumo wa bluetooth (Wireless Speaker).

Watakaoilipia Tecno Camon 16s

Watakaoilipia Tecno Camon 16s kupata zawadi mbalimbali

Taarifa hiyo imeeleza kwamba  promosheni hiyo inaanza rasmi tarehe 2 Novemba 2020 na itadumu kwa muda wa siku saba yaani wiki moja mpaka tarehe 9 Novemba 2020. Katika kipindi hiki cha wiki moja mteja atatakiwa kutembelea maduka yaliyochaguliwa kufanya promosheni hiyo na kuweka oda ya mapema yaani ku Pre-order.

Sifa na uwezo wa TECNO CAMON 16s unaofahamika hadi sasa:

  • kamera nne nyuma huku kamera yake kuu ikiwa ni ang’avu yenye MP48,
  • Screen kubwa ya inchi 6.6
  • Kiwango cha diski uhifadhi wa GB 128 ROM ikija na RAM ya GB4.
SOMA PIA  ZTE Axon M: Simu yenye screen mbili, ni simu inayoenda kinyume na tulichozoea

Kufuatia ujio wa simu hii mpya, kampuni ya TECNO imechagua takribani maduka 35 nchini, kufanya promosheni ya Pre-oder katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Mbeya, Kagera, Kilimanjaro na Dodoma ili kuwasaidia wateja wake wa mwanzo kupata simu hii bab kubwa kwa bei nafuu pamoja na zawadi, hivyo mteja anaweza kufanya Pre-order katika maduka yaliyoorodheshwa hapo chini pamoja na namba za kuwasiliana moja kwa moja na wahusika. Pia mteja anaweza ku-Pre-order kwa kutumia link hii: Pre Order Camon 16s.

SOMA PIA  iPhone 11 ndio simu iliyouzika zaidi mwaka 2020

 

MKOA DUKA NO YA SIMU
 

DAR ES SALAAM

Mlimani city, China Plaza, Mobimart, Hyatt, Inobit, RAM 3, RAM 4, Vodacom Mlimani City, Mashreq 0654843687

0654 304803

 

MWANZA

Exclusive Jambo Shop, Mbaraka Shop, TECNO Exclusive Katoro Shop, J.B mobile, FAHARI shop 0719083413

0753144128

ARUSHA Isacky Technology, Happy Shop 0715092100
DODOMA TECNO Exclusive Pablo shop 0764161011
MOSHI TECNO Exclusive Totolee 059392893
MBEYA TECNO Shop Mbeya, BM shop 0758442496
BUKOBA TECNO Exclusive Bukoba Shop 0719083413

0753144128

Je ushawahi kununua simu yeyote kupitia mfumo wa malipo ya kabla (Preorder)?

Comrade Mokiwa

Comrade Mokiwa

Muanzilishi wa Teknokona na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania