fbpx

Wanasayansi: Goli la Messi lina uwezo wa kutikisa jiji zima la Barcelona

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Wanasayansi waliweka vifaa vya kupima tetemeko la ardhi katika uwanja wa Nou Camp na kufanikiwa kupima mitetemeko ya ardhi kila nyota wa timu ya Barcelona, Lionel Messi anapofunga goli.

Wakati Lionel Messi anapofunga goli mji wa Barcelona hutetemeka na athari ya mabao yake huonekana katika data kila wakati mashabiki wanaposheherekea kwa kuruka juu na chini uwanjani.

Vipimo hivyo vilidhihirika wakati Barcelona ilipofanya miujiza ya kutoka nyuma na kuishinda klabu ya Paris Saint Germain katika kombe la klabu bingwa Ulaya msimu uliopita.

kutikisa jiji

Huku wakiwa 4-0 katika awamu ya kwanza ya makundi ya mtoano, timu hiyo ilifunga bao la dakika za lala salama na kupata ushindi wa jumla ya 6-5 nyumbani hivyo kusababisha jiji kutikisika kama takwimu zinavyoonyesha pichani.

Tetemeko la ardhi linalosababishwa na kandanda limejadiliwa katika kongamano la sayansi la Ulaya huko Vienna, Austria. Ni kazi ya Jordi Diaz na wenzake katika taasisi ya sayansi ya ardhini.

Bw. Diaz na wenzake walibaini kuwa hata kwenye matamasha makubwa ya muziki mathalani tamasha la Bruce “The Boss” Springsteen au U2 yaliyowahi kufanyika katika uwanja wa Nou Camp yana uwezo wa kulitikisa jiji zima la Barcelona.

kutikisa jiji

Sababu kubwa ya magoli ya Messi/matamasha ya muziki wa kurukaruka (rock) kuweza kusababisha mtkisiko jiji zima ni kwa sababu watu huwa washangilii tu bali huwa wanacheza pia.

Kipimo hicho cha Diaz kimewekwa mita 500 kutoka uwanja huo na kifaa hicho kimekuwa kikitumika kupima hali inavyokuwa wakati wa foleni barabarani, treni zinapopita.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.