fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

apps

Wafanyakazi Wa Zamani Wa WhatsApp Waja Na HalloApp!

Wafanyakazi Wa Zamani Wa WhatsApp Waja Na HalloApp!

Spread the love

HalloApp ni mtandao wa kijamii wenye sifa ya kipekee ukilinganisha na mitandao mingine, mtandao huu umeanzishwa rasmi na wafanyakazi wawili wa (mwanzo) zamani kabisa wa WhatsApp.

Mtandao huu wa kijamii kwa sasa unapatikana Apple’s App Store na Google Play

HalloApp

HalloApp

Dhima nzima ya mtandao huu ni kuwaunganisha karibu zaidi watu wa kundi ambalo wanafahamiana vizuri kama vile marafiki na familia

Kama WhatsApp tuu ili kuweza kuwasiliana na watu hao lazima uwe na namba zao za simu ili kuweza kufanikisha maongezi nao katika HalloApp.

Muonekano Wa HalloApp..

Muonekano Wa HalloApp..

Meseji ambazo zinatumwa na kupokelewa zinakuwa na usalama wa hali ya juu (encrypted) na vile vile kunakuwa hakuna matangazo ya aina yoyote ndani ya mtandao huo.

SOMA PIA  Snapchat Waanzisha Ma'Group' Na Vipengele Vingine, Sasa Chat Mpaka Na Watu 16!

Wawili hao nyuma ya mtandao huo ni Neeraj Arora na Michael Donohue amabo wote walikua katika nafasi za juu za WhatsApp kabla haijanunuliwa na Facebook.

Muonekano Wa HalloApp

Muonekano Wa HalloApp

Kwa sisi TeknoKona tunapenda kuona mtandao huu unazidi kukuwa na kuleta mapinduzi makubwa katika mitandao ya kijamii katika kuhakikisha tunapata huduma bora zaidi

SOMA PIA  KeyFree Watarajia Kusema Kwaheri Kwa Funguo Za Gari!

Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, niambie mtandao wa HalloApp umeupokeaje?

Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Wa TeknoKona Kila Siku Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania