fbpx

Volvo Kuhamia Katika Kutengeneza Magari Ya Umeme!

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Volvo ni kampuni kubwa sana duniani ambalo linajihusisha na utengenezaji na uuzaji wa magari. Kampuni hilo kutoka Sweden, limetoa taarifa ya aina yake ambayo itabadilisha teknolojia kwa ujumla.

Volvo imesema mpaka kufikia 2021 itakua tayari imeshatoa magari yake ambayo yanatumia umeme. Magari ambayo yatatoka yatakuwa ni ya aina tano lakini mpaka sasa bado hatujajua ni aina gani za magari hayo.

Ukiachana na magari kutegemea nishati ya sehemu moja kwa mfano kama ni la mafuta kutumia mafuta tuu au kama ni la umeme kutumia umeme tuu, pia kuna magari yatatolewa katika kipindi cha baadae ambayo yatakuwa yanatumia nishati zote mbili.

Aina za magari ambayo yatakuwa yanatumia umeme zitawekwa wazi na kampuni kati ya mwaka 2019 na 2021.

Kampuni Ya Volvo

Kwa sasa sio kama kampuni itakuwa na mpango wa kuacha kutengeneza magari ya kawaida (ya nishati ya mafuta) bali itakua inaendelea mpaka magari hayo yatakapofika.

Kumbuka kwa sasa kampuni ambayo ni tishio katika teknolojia ya nishati ya umeme katika magari ni Tesla Motors. Kampuni ya Tesla kwa sasa imejipanga vizuri katika kumpokea mpinzani huyo na inaendelea fanya kazi kama kawaida huku ikijiboresha zaidi.

Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini sehemu  ya comment. Unaonaje maendeleo ya kampuni ya volvo kwa kuja na nishati ya umeme katika magari?

Kumbuka Kutembelea  Mtandao Wako Pendwa Wa TeknoKona Kila SIku Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.