Kampuni nguli katika utengenezaji wa magari, Volkswagen imeingia katika mgogoro mwingine baada ya makampuni yanayoiuzia vifaa kwa ajiri ya kutengeneza magari kugoma.
Makampuni ambayo yanaiuzia VW vifaa mbalimbali kwaajiri ya utengenezaji wa magari huko Ujerumani yameingia katika mgomo yakilazimisha kampuni hiyo kuwalipa fidia baada ya moja kati ya mikataba yake na VW kuvunjwa.
Msemaji wa Volkswagon anasema kwamba mahakama imekwishatoa amri kuyaamrisha makampuni hayo kuendelea na huduma ingawa vyanzo vya habari hii havikuweza kupata kauli kutoka katika umoja wa makampuni hayo.

Hatua hii imeiathiri kampuni hii kiasi cha kupunguza uzalishaji katika viwanda vyake nchini Ujerumani, tayari Volkswagen wamekwisha pata hasara kubwa baada ya skendo yao ya uchafuzi wa mazingira ambayo ilisababisha kampuni hiyo kulipa karibu dola za kimarekani bilioni 18.
Taarifa hii imeripotiwa na mtandao wa BBC.