fbpx

Vodacom Tanzania wana huduma mpya

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Vodacom Tanzania wamekuwa wakija na huduma mbalimbali kama njia ya kuvutia wateja ambao tayari wanatumia mtandao huo au hata wale ambao wanashawishika na kuamua kujiunga nao.

Makampuni yanayojishughulisha na utoaji huduma za mawasiliano nchini Tanzania yamekuwa katika ushindani kila leo na mmoja akitoa hudma fulani basi na mwingine yupo kwenye maandalizi ya kutoa ya kwake pia.

Ukuzutathimini huduma mbalimbali ambazo kamuni za simu wanatoa utaona kuwa hazitofautiani sana na hasa kuwa na mantiki ileile ukitazama huduma ya ‘JIHUDUMIE‘ kutoka Tigo Tanzania na siku si nyingi zilizopita Vodacom Tanzania wamezindua ‘Naweza na Vodacom‘ ambayo itawawezesha wateja wao kufanya mambo yafutatayo:-

  • kuzuia/kurudisha muamala uliokosewa,
  • kuweza kurudisha nywila/nenosiri lililozuliwa au mteja amesahau,
  • kuweza kupata usaidizi kupitia ujumbe wa sauti uliorekodiwa kulingana na kile ambacho wateja wanasumbuka nacho mara kwa mara.

    Vodacom Tanzania

    Huduma ya ‘Naweza na Vodacom’ inapatikana ndani ya menyu ya M-Pesa (*150*00#).

Pengine kwa ujio wa huduma ya “Naweza na Vodacom”  itapunnguza misururu kwenye maduka ya Vodacom wakitafuta msaada zaidi wa matatizo ambayo wanakumbana nayo kwenye mtandao wa simu husika au hata kuweza kutumia kurasa za kwenye mitandao ya kijamii, programu tumishi-My Vodacom, M-Pesa kutatua tatizo na hayo ndio mambo ya kidijiti!.

Chanzo: Vodacom Tanzania

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Undani wa Sony Xperia Ace #Uchambuzi
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.