fbpx

VLC haipatikani kwa baadhi ya simu za Huawei

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Programu tumishi ya VLC imekuwa ni moja ya kitu muhimu kuwepo kwenye simu janja za watu kutokana na uzuri wake kuwezesha kuangalia picha za mnato kwa wepesi kabisa na hivyo kuwa na idadi kubwa ya watu walioiweka kwenye simu zao.

Mambo ni tofauti kidogo kwa baadhi ya simu rununu za Huawei; P8, P10 na P20 kwa kutopatikana kwa programu hiyo kwenye soko la programu tumishi kwa simu za Android na hii ni kwa sababu wahusika wamezuia wenye simu hizo kupakuwa VLC.

Watumiaji wa simu za Huawei wamekuwa wakiipa sifa ya nyota moja kwenye sehemu ya kutolea maoni kwa kosa ambalo VLC haihusiki kabisa. Simu hizo zinaelezwa kutumia kiasi kikubwa cha chaji na hivyo kuamua kusitisha programu tumishi zinazofanya kazi upande wa nyuma (background apps) ikiwemo na VLC.

Ukisitisha VLC kufanya kazi kwa ule upande wa nyuma moja kwa moja unaathiri ufanisi wa programu tumishi ya VLC kwenye simu.

baadhi ya simu

Kitendo cha VLC kulaumiwa kuwa ni chanzo cha kumaliza chaji na kutoa maoni mabaya kimewakera wahusika na kuamua kutopatikana kwa baadhi ya simu za Huawei.

Programu ya VLC haipatikani kwenye Play Store tu lakni watu wanaweza kuipakuwa katika mfumo wa APK na kuiweka kwenye simu zao.

yanzo: 9To5Google, The Verge

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Xiaomi Mi Mix 3 yenye 5G imetoka
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.