fbpx
DSTV, King'amuzi, Maujanja, Teknolojia

Ving’amuzi vya DSTV na sehemu ya kuchomeka USB/Flash

vingamuzi-vya-dstv-na-sehemu-ya-kuchomeka-usb-flash
Sambaza

Ving’amuzi vya DSTV ni moja ya visimbuzi ambavyo watu wengi kwenye nchi za Afrika wanavitumia kuweza kupata chaneli mbalimbali duniani kwa lengo la kuhabarika, kuelimika, kuburudika, n.k ambapo teknolojia imeendelea kubadilika mpaka kufikia kuwa na sehemu ya kuchomeka USB ama flash.

Nina imani kama utakuwa ni mtu unayependa kukijua kifaa cha kielekroniki kabla ya kukiunganisha kwenye umeme basi utakuwa umeona  kuwa bidhaa hiyo ina sehemu ambayo inaruhusu kuchomeka memori ya nje au kwa Kiingereza “Flash Disk Drive” au waya unawezesha kuchaji simu, tabiti.

INAYOHUSIANA  Messenger Rooms kwenye WhatsApp
Kuchomeka USB
Kuchomeka USB: Sehemu ya nyuma kwenye king’amuzi cha DSTV.

Sasa kuna kitu kimoja kwenye king’amuzi cha DSTV kikawa kimekuacha na maswali kidogo; suala la kwamba ukichomeka memori ya zida kwa ajili ya kuweza kuangalia sinema, picha jongefu za muziki na mengineyo inakuwa haisomi lakini ukichomeka waya wa kuchaji simu (USB) kwenye rununu umeme unaingia. Je, ni kwanini ving’amuzi vya DSTV havikubali flash disk?

Jibu ni DSTV hawajaruhusu memori ya ziada (FDD) kuweza kutambulika kwenye king’amuzi LAKINI inawezekana kutumia sehemu hiyo kwa ajili ya kuchaji simu pamoja na vifaa vinginevyo vya kiganjani.

HIyo ndio JE, WAJUA?! Sasa tufahamu tuu tunaweza kuchaji rununu, tabiti kwenye king’amuzi cha DSTV na si vinginevyo. Sisi ndio TeknoKona, tufuatilie kila leo kwa habari mbalimbali zinazohusu teknolojia.

Chanzo: DSTV

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|