fbpx

Android, apps, iOS, Teknolojia, Telegram

Uwezo wa kuficha utambulisho wa kiongozi wa kundi kwenye Telegram

uwezo-wa-kuficha-utambulisho-wa-kiongozi-wa-kundi-kwenye-telegram

Sambaza

Telegram ni programu tumishi ambayo ina vitu vingi vizuri na maboresho mengi ndio huwa yanaonekana huko kwanza lakini si maarufu kwa watu wengi lakini wanaotumia basi wanafurahi sana!.

Ukizungumzia uwezo wa kuwa na washiriki hata elfu tano au zaidi, mazungumzo ya siri, kutuma kitu cha hata GB 2 pamoja na vitu vingine vingi basi pasi na shaka utakuwa unailenga Telegram ambapo juzi juzi tuu wameweka kipengele cha kuweza kupiga simu katika mfumo wa picha jongefu. Mbali na hayo kuna maboresho ambayo Telegram imeyafanya na kuifanya iwe programu tumishi inayovutia ingawa haijulikani kwa wengi. Vitu vipya ni:

Kuficha utambulisho wa kiongnozi wa kundi

Kwenye Telegram ukitaka kuanzisha kundi basi kuna watu wawili ambao ni muhimu sana; mmiliki na kiongozi wa kundi. Sasa katika maboresho ambayo Telegram imeyafanya ni kuwezesha kuficha taarifa za kiongozi wa kundi (wanakuwa hawajulikani) iwapo watruhusu kipengele cha “Batman mode” ndani ya mpangilio wa kiongozi wa kundi husika. Kipengele cha Batman kinafanya viongozi wa kundi kutoonekana kwenye orodha ya watu kwenye kundi husika.

INAYOHUSIANA  Simu milioni 900 za Android hatarini kudukuliwa

Uwezo wa kutafuta kitu kulingana na muda, jina

Kitu kingine ambacho kimeboreshwa ni jinsi gani namna ya kutafuta kitu ndani Telegram ilivyoboreshwa; unaweza kutafuta kitu kulingana na tarehe, wakati, n.k mathalani ukiandika “October 1” au “Yesterday” basi itatafuta na kuleta majibu kulingana ulichokiandika kwenye kipengele cha kutafuta.

Uwezo wa kutoa maoni kwenye chaneli

Wengi wetu tunafahamu kuwa inawezekana kutengeneza chaneli ndani Telegram ambapo maudhui yake ni tofauti kabisa na kundi. Kwenye maboresho yaliyofanywa Telegram wameongeza kipengele cha mtu kuweza kutoa maoni (comment) ndani ya chaneli husika kwa zenye makundi yanayoruhusu majadiliano; kitufe cha kutoa maoni kinaonekana kwa washiriki wote kwenye chaneli pamoja na kundi lililorusu majadiliano. Na hata kama mtu si mshiriki kwenye kundi ambalo limeruhusu majadiliano atapata taarifa fupi kuhusu ambacho kimejibiwa na wengine.

INAYOHUSIANA  Tesla Inaufanyia kazi mfumo wa magari yake kujiendesha yenyewe
kiongozi wa kundi
Maboresho mapya kwenye Telegram: Uwezo wa kutafuta kitu, vikatuni vipya, maoni ya watu kutoka kwenye chaneli.

Telegram imeboresha mambo mengine madogo madogo kama kuonyesha/kupicha kicharazio, kuchagua muonekano wa giza/mwanga utokee muda gani, n.k. Unachotakiwa kufanya ni kupakuwa masasisho ya programu tumishi husika kutoka kwenye App Store au Playstore.

Vyanzo, Gadgets 360, EN24.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Reply your comment

Your email address will not be published. Required fields are marked*