fbpx

Kamera za Huawei P30 Pro: Uwezo wake kuzoom ni hatari (video)

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Kamera za Huawei P30 Pro zinafanya simu hiyo kuwa moja ya simu zenye uwezo mkubwa zaidi wa picha/video zenye ubora wa hali ya juu.

Kamera za Huawei P30 Pro zina uwezo wa kuzoom kwa mfumo wa ‘optical’ mara 5 (5x Optical zoom – yaani zoom inayohusishwa usogeaji wa lense kwenye kamera). Wakati katika mfumo wa kuzoom kidigitali ni wa mara 50 (50x digital zoom).

huawei p30 pro

Huawei P30 Pro

Huawei p30 pro

Simu ya Huawei P30 Pro eneo la kamera

Mjumuisho wa teknolojia hizi mbili unaifanya simu hiyo kuwa na uwezo wa kupiga picha za mbali katika ubora/kiwango cha hali ya juu sana.

Katika kamera za simu mara nyingi simu zina ‘digital zoom’ na si ‘optical zoom’, digital zoom kiuhalisia kuna kuwa hakuna lens zozote zinazojisogeza kwenye kamera kuweza ku’zoom’ bali kinachofanyika ni kamera yako kukata eneo lile linalopazunguka pale unapotaka kupapiga picha.

simu-asus-zenfone-zoom-4

Hii inafanya ubora wa picha yaani ‘quality’ kupungua. Ili kuwa na uwezo halisi wa optical zoom lazima kuwe na lens zinazosogea na kujirudisha pale unapozoom ili kuhakikisha unaendelea kuwa na picha ya ‘quality’ nzuri hata pale unapozoom.

Katika video iliyowekwa mtandaoni huko nchini Uchina na mtumiaji aliyetumia simu ya Huawei P30 Pro akiwa juu ghorofani- kamera ya simu hiyo imeonesha uwezo mkubwa wa kuweza kuzoom hadi kusoma herufi/alama ndogo zilizokuwa kwenye gemu watu walikuwa wanacheza eneo la chini na mbali kidogo kutoka kwenye jengo alilokuwa mpiga picha.

INAYOHUSIANA  Marekani kupunguza vikwazo kwa Huawei, Huawei wasema hawana uhakika bado

Jionee uwezo huo kupitia video hiii hapa;

Soma zaidi makala yetu kuhusu simu za Huawei P30 na Huawei P30 Pro hapa -> Huawei P30: Hizi hapa simu mbili mpya za Huawei za P30 na P30 Pro

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.