WhatsApp Desktop imekuwa ni mkombozi wa watu wengi tuu ulimwenguni ambao kazi zetu zinategemea matumizi ya kompyuta hivyo kufanya uwezekano wa kushika simu na kujibu jumbe kuwa mdogo.
Kwa wale ambao tunatumia WhatsApp Desktop kwenye maisha yetu ya kila siku tunafahamu jinsi ambavyo imetusaidia kuokoa vifurushi vyetu vya intaneti kwani si lazima simu iwe na kifurushi cha intaneti kwenye simu ili mtu aweze kupokea/kujibu jumbe za WhatsApp kupitia kompyuta ambayo ni lazima iwe imeunganishwa na intaneti.
Njia hii ya mawasiliano ya WhatsApp imekuwa ikifanyiwa maboresho kila pale ambapo inaonekana ni wakati sahihi kupeleka masasisho hayo kwa watumiaji wake. Binafsi ni mtumiaji wa WhatsApp Web/desktop na hivi karibuni nimeona maboresho ambayo yamefanyika kwa kufanya uwanja kuwa mpana kwa mtumiaji kuweza kukiangalia kwa ukubwa kile ambachoanataka kumtumia mhusika.

WhatsApp Desktop imerahisisha mambo mengi ambayo kwa kiasi fulani unaweza usijutie iwapo itatokea ukasahau simu yako nyumbani huku asilimia kubwa ya watu unaofanya nao mawasiliano ni kwa njia ya WhatsApp na unaweza ukafanikisha hilo iwapo utakuwa na kompyuta.
Yapo mengi ambayo tutazidi kuwahabarisha kuhusiana na hiki ambacho nimekizungumzia leo. Hili la maboresho ya uwanja mpana ni sehemu tuu ya mengi ambayo bado hujayahafamu. Endelea kutufuatilia na hakika utafurahi.
Chanzo: WaBetaInfo
No Comment! Be the first one.