fbpx
iOS, Teknolojia, whatsapp

WhatsApp: Mbioni VoiceNote Kuanza Kujibika Katika Eneo La Notification! #iOS #iPhone

utaweza-jibu-voice-note-whatsapp-katika-notification
Sambaza

WhatsApp ni mtandao  kubwa sana wa kijamiii, watumizi wake wanazidi ongezeka siku hadi siku! Hakika ni moja ya njia rahisi sana ya kuwasiliana na watu duniani kote. Mara kwa mara mitandao hii ya kijamii huwa inatoa maboresho mbali mbali ili kujihakikishia inazidi kukua na kuendelea zaidi.

Kupitia ukurasa wa Twitter WABetaInfo kama kawaida yao wamekuwa mara kwa mara wakitoa fununu na taarifa mbali mbali kuhusu matoleo mapya na vipengele vipya katika mtandao wa WhatsApp

INAYOHUSIANA  Waiba Tsh Bilioni 27.9 katika zaidi ya ATM 1,400 ndani ya masaa 3!

Japokuwa ni wazi mtandao huo unakataa kwamba hauna uhusiano wa moja kwa moja na mtandao wa WhatsApp lakini mara kwa mara wamekua wakitoa taarifa hizi za matoleo na vipengele bila kukosea

@WABetaInfo walituma tweet hii

Kwakuwa na picha ambayo wameituma imeonesha kifaa cha iOS hivyo basi inasemekana kipengele hiki kinaweza anza kuonekana katika vifaa janja kutoka Apple kwanza alafu baadae labda ndio nao Android wataweza anza furahia huduma hii.

INAYOHUSIANA  Kutafuta kitu mtandaoni kupitia WhatsApp

Lakini bado hakuna uhakika sana, nani anajua zaidi bwana? unaweza shangaa kikatoka kwa wote mara moja. cha muhimu ni kusubiri mpaka hapa toleo hili litakapopatina katika vifaa vyetu

Muonekano Wa Kipengele Hicho Katika Toleo Jipya Katika Kifaa Cha iOS
Muonekano Wa Kipengele Hicho Katika Toleo Jipya Katika Kifaa Cha iOS

Kingine ni kwamba hii inaweza ni moja wapo ya vipengele vingi ambavyo vipo mbioni kuja katika toleo la WhatsApp lijalo…. tujiandae tuu…

Ningependa kusikia kutoka kwako, hii umeipokeaje? niandikie hapo chini katika sehemu ya maoni… tafadhali usiache kutembelea mtandao wako pendwa wa TeknoKona kila siku kwani daima tupo nawe katika sayansi na teknolojia kwa ujumla.

Umeshawahi Kuingia huku?

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Hashdough

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com