WhatsApp ni mtandao kubwa sana wa kijamiii, watumizi wake wanazidi ongezeka siku hadi siku! Hakika ni moja ya njia rahisi sana ya kuwasiliana na watu duniani kote. Mara kwa mara mitandao hii ya kijamii huwa inatoa maboresho mbali mbali ili kujihakikishia inazidi kukua na kuendelea zaidi.
Kupitia ukurasa wa Twitter WABetaInfo kama kawaida yao wamekuwa mara kwa mara wakitoa fununu na taarifa mbali mbali kuhusu matoleo mapya na vipengele vipya katika mtandao wa WhatsApp
Japokuwa ni wazi mtandao huo unakataa kwamba hauna uhusiano wa moja kwa moja na mtandao wa WhatsApp lakini mara kwa mara wamekua wakitoa taarifa hizi za matoleo na vipengele bila kukosea
@WABetaInfo walituma tweet hii
I leave this here.
Yes, it's a push notification with an incoming voice message, on iOS.
It will be available in future (maybe in a major update with other features?) pic.twitter.com/eSm55GxFuO— WABetaInfo (@WABetaInfo) July 18, 2019
Kwakuwa na picha ambayo wameituma imeonesha kifaa cha iOS hivyo basi inasemekana kipengele hiki kinaweza anza kuonekana katika vifaa janja kutoka Apple kwanza alafu baadae labda ndio nao Android wataweza anza furahia huduma hii.
Lakini bado hakuna uhakika sana, nani anajua zaidi bwana? unaweza shangaa kikatoka kwa wote mara moja. cha muhimu ni kusubiri mpaka hapa toleo hili litakapopatina katika vifaa vyetu
Kingine ni kwamba hii inaweza ni moja wapo ya vipengele vingi ambavyo vipo mbioni kuja katika toleo la WhatsApp lijalo…. tujiandae tuu…