Utafiti uliotolewa hivi karibuni unaonesha asilimia kubwa ya upatikanaji habari au taarifa mbalimbali kwa watu wengi hutegemea zaidi mitandao ya kijamii.
Hivi karibu kituo cha utafiti cha Pew kilifanya uchunguzi huko Amerika kwa watu wazima 4,971 na kubaini chanzo chao cha habari hutegemea ni zaidi mitandao ya habari.
Kutoka utafiti huo walichapisha ripoti ya matokeo na ilionesha kuwa 67% ya wamarekani wanapata habari kupitia mitandao ya kijamii.
Jambo la kuvutia zaidi lililotoka katika ripoti hiyo ni kuwa 55% ya watu wenye umri wa miaka 50 au zaidi walisema kuwa wanapata habari kutoka kwenye tovuti za vyombo vya habari.
Kwa kawaida ungefikiri kuwa kizazi cha vijana ndio hutegemea mitandao ya kijamii kupata na kufuatilia habari mbalimbali.
Kadhalika Kwa mujibu wa ripoti ya mwezi Juni mwaka huu iliyotolewa na taasisi ya utafiti wa uandishi wa habari ya Reuters ilieleza kwamba zaidi ya nchi 30 zilionesha kwamba WhatsApp imekuwa chanzo cha habari kwa watu wengi.
Hata hivyo changamoto kubwa ya mitandao ya kijamii kwa watu wengi kuwa na wasiwasi wa kupata taarifa zisizo za kweli ambazo zimekuwa zikizushwa na zikisambazwa kila siku.