fbpx
Betri, IPhone

Using’ate betri: Mtu kajifunza kwa njia mbaya, asababisha mlipuko

usingate-betri-mtu-kajifunza-kwa-njia-mbaya-asababisha-mlipuko
Sambaza

Using’ate betri kwa sababu yeyote ile! Kuna mtu nchini China alifikiri anaweza kuangalia kama betri ni feki au la kwa njia ya kung’ata. Kilichotokea hatosahau kamwe.

using'ate betri la simu
Betri la simu ya iPhone lalipuka dukani baada ya kung’atwa

Mwanaume huyo alienda kwenye duka la elektroniki katika jiji la Nanjing kwa lengo la kubadili betri la simu yake ya iPhone, ila baada ya kuoneshwa betri jipya linalotakiwa kuwekwa kwenye simu yake yeye alitaka kujihakikishia ubora wa betri hilo. Aliamini betri likiweza kuminyika sana baada ya kung’atwa basi halitakuwa betri orijino, ila sasa amejifunza kutotumia njia hiyo tena.

INAYOHUSIANA  iPant? Hii Kwa Ajili Ya iPhone 6 Plus!

Baada ya mwanaume huyu kuling’ata betri hilo na kujiridhisha baada ya muda betri lililipuka na kusababishwa hatari ndani ya duka hilo ingawa taarifa zinaonesha kwa bahati nzuri watu walisalimika.

Kulingana na jinsi mabetri ya Lithium-ion yanavyotengenezwa kuna sehemu za ndani ya betri hazitakiwa kugusana kabisa. Kugusana kwake kutaanzisha mchanganyiko cha kemikali unaosababisha joto kubwa (linaweza kufika hadi nyuzi 500 za Sentigredi), joto hili ndio linakuja kusababisha mlipuko wa betri husika au kama joto si la juu sana basi betri linaweza likawaka moto tuu.

INAYOHUSIANA  Pengine iPhone Itaachana Na 'Touch ID' Na Kuja Na 3D Face Scanning!

Angala video ya tukio hilo hapa chini

Asante kwa kuendelea kusoma TeknoKona, ungana nasi pia kupitia www.facebook.com/teknokona na www.twitter.com/teknokona 

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share
Tags: ,

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |