fbpx

Ushirikiano mzuri kati ya Dropbox na Google Drive

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Tunaopenda kuhifadhi vitu “Kusikojulikana” bila shaka tutakuwa tunafahamu kazi ya Dropbox na Google Drive kutokana kwa namna moja au nyingine tumeshawahi kutumia vitu hivyo ili kuweza kutunza vitu vyetu na kuweza kuvifikia wakati wowote ule.

Katika teknolojia ya leo inatulazima kuwa na sehemu mbalimbali za kuweza kutunza vitu vyetu ili hata pale linapotokea janga la kupoteza vitu fulani basi unaweza ukavipata sehemu nyingine (iwapo ulivihifadhi huko) na hapo ndipo umuhimu wa Dropbox au Google Drive unapoonekana.

Sisi ambao tunapenda kutumia mbadala wa kutumia Google Drive kuandaa vitu kwa ajili ya kazi zetu imerahisisha vitu vingi lakini ilikuwa ni changamoto iwapo ukiamua kumsambazia mtu ambae anatumia Dropbox, hilo sasa limepatiwa ufumbuzi kwani inawezekana kutengeneza Google Docs, Sheets na Slides ndani ya Dropbox.

Google Drive na Dropbox

Uwezo wa kutengeneza nyaraka mbalimbali ndani ya Dropbox hivyo kufanya mawasiliano mazuri  kati ya programu hizo mbili.

Kwa ushikiano huo hii inamanisha mtu ataweza kuhariri nyaraka yoyote iliyotengenezwa kutoka kwenye Google Drive, kuhariri, kuandika maoni kuitumia bila kuomba ruhusa kwa aliyekutumia kitu ambacho ilikuwa kama bugdha kwa watumiaji wa Dropbox.

INAYOHUSIANA  Apps na Programu za Google Drive na Google Photos zatenganishwa

Kwa hivi sasa kipengele hicho kinapatikana kwa wale wanaotumia “Dropbox for Business” lakini kitaweza kupatikana kwa wote ndani ya siku za usoni. Vipi wewe msomaji wetu, umefurahishwa na ushirikiano huo? Tupe maoni yako.

Vyanzo: Thech The Lead, FoneArena

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.