fbpx
apps, Maujanja, Teknolojia

USB OTG ni nini? Je simu yako ina #teknolojia hii? – Fahamu

usb-otg-ni-nini-fahamu-zaidi
Sambaza

Teknolojia ya USB ni moja ya teknolojia zinazotumika zaidi katika suala zima la uhamishaji wa mafaili na uunganishwaji wa vifaa tofauti tofauti vya elektroniki. USB OTG inakuwezesha kuunganisha vitu kama USB Flash Drive, keyboard n.k na simu yako.

USB On-The-Go (OTG) ni mfumo wa kielektroniki unaoruhusu vifaa vya elektroniki ambavyo si kompyuta kuweza kusoma data kutoka vifaa vingine vya elektroniki bila uhitaji wa kompyuta.

usb otg
Waya (cable) wa USB OTG – Upande mmoja unaweza chomekwa kwenye simu au tableti alafu upande wa pili unaweza tumiwa kuchomekwa keyboard, kipanya au kifaa kingine chochote cha elektroniki kwa njia ya USB

Mambo yanayowezekana kutokana na teknolojia ya USB On-The-Go

Unaweza kusoma data kama vile miziki, video na mafaili mengine kutoka kwenye USB Flash Drive.

Pia unaweza tumia ‘Vichezea Magemu’, yaani ‘Game controllers’ kimombo ili kuweza kucheza magemu ya kwenye simu janja au tableti yako kwa urahisi.

INAYOHUSIANA  Simu za Huawei kukosa apps za Facebook, WhatsApp na Instagram

Je kifaa chako kina teknolojia ya USB OTG

Ingawa teknolojia hii inawezekana kwenye vifaa vingi vya kisasa vya Android (simu na tableti) pia inaweza tumika kwenye vifaa vingine mbalimbali kama vile baadhi ya simu za Windows. Hadi sasa hakuna dalili ya Apple kuiruhusu katika simu zao za iPhone.

Njia ya haraka ya kufahamu kama simu au tableti yako imekuja na teknolojia hii ni kuangalia alama za kiteknolojia zilizokwenye boksi la simu au tableti hiyo. Kama kuna nembo iliyo hapa chini basi teknolojia hii imekuja na kifaa chako.

INAYOHUSIANA  Google kuchunguzwa na chombo cha Biashara cha Umoja wa Ulaya
usb otg
Logo ya teknolojia ya USB OTG

Pia simu na tableti nyingi za kisasa zilizotoka katika kipindi cha miaka miwili hivi zimekuja na teknolojia hiyo.

Njia nyingine kwa watumiaji wa simu za Android ni kupakua app ya USB OTG Checker. App hii inasaidia kuitambua simu yako na programu endeshaji yake na kisha kukuambia kama simu hiyo imekuja na uwezo huo – USB OTG.

Je vifaa vya USB OTG unaweza vipata wapi?

Unaweza nunua ‘cable’ za USB OTG kwenye maduka ya elektroniki, si yote yanaweza kuwa nayo ila tayari zinapatikana kwenye maduka mengi. Uangaliaji wetu wa haraka haraka kwenye mtandao wa mauzo ya kimtandao – Jumia tumeweza kuona zinapatikana.

INAYOHUSIANA  Toleo la Google Play Store linasababisha simu kuisha chaji haraka
usb otg
Adapta ya USB OTG ikiwa inauzwa kwa bei ya Tsh 7,000/= tuu kupitia mtandao wa Jumia. Unaweza pia kuangalia kwenye maduka ya elektroniki karibu na ulipo na unaweza kuzipata pia.

Pia tayari kuna USB Flash diski zinazokuja na teknolojia ya USB OTG upande wa pili na hivyo zinaweza kuchomekwa kwenye simu na mtu kuweza kuhamisha mafaili moja kwa moja kutoka kwenye flashi diski hiyo kwenda kwenye simu n.k.

App ya USB Checker – Google PlayStore

Je wewe ushawahi kutumia teknolojia hii? Tuambie maoni yako.

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTubeTelegram na Google Plus

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |