Wasimamizi wa masuala ya mawasiliano nchini Urusi wametishia kuufungia mtandao wa Facebook nchini humo kufikia mwaka 2018.
Kwa mujibu wa habari, sheria ya Urusi huyataka makampuni yote kutoka nje kuhifadhi data zake nchini humo.
Mtandao wa Facebook umekubali kupeleka mbele ya kamati ya bunge la Marekani data za watumiaji na watangazaji matangazo wa Urusi waliofanya hivyo kipindi cha uchaguzi wa Marekani.

Kiongozi wa shirika la mawasiliano nchini humo Alexander Zharov amesema kuwa kutokana na sheria ya Urusi ya mwaka 2014, Facebook inapaswa kuhifadhi data zake nchini humo au ikubali kufungiwa.
Alexander Zharov vilevile katika mahojiano amesema kuwa Twitter imekubaliana na sheria hiyo na imeahidi kufanya hivyo ifikapo katikati ya mwaka 2018.