fbpx
simu, Teknolojia

Je, Urefu Wa Chaja Unaathiri Kiwango Cha Chaji Inayoingia Katika Kifaa Chako?

urefu-wa-chaja-unaathiri-chaji
Sambaza

Watu wachache sana wanaielewa teknolojia, wengi wetu hatuijui vizuri. Hivyo basi inatufanya tuwe na maswali kadha wa kadha kuhusiana na mambo Fulani Fulani hivi yanayohusu teknolojia.

Ntakua mkweli, Mzee wangu ambae kasoma sana na pia ni muhasibu na mtaalamu wa mambo hayo aliniuliza “Hivi Flash inapata Virus Kama mfuniko wake ukiwa wazi?” na nlishangazwa na swali hili kwa kuwa mkweli

Lakini kadri muda ulivyoenda nligundua kuwa kuna maswali ya ajabu ajabu. Kwa mfano ukiingia katika tovuti ya Yahoo Answers unaweza ukagundua kuwa kuna maswali ya kijinga sana katika dunia hii na ni vizuri kuwa nayo. Kupitia maswali ya namna hii ndio mtu unaweza jifunza zaidi.

Kwa mfano kuna maswali mawili ambayo nimeyashuhudia..

  • Mtu wa kwanza kauliza “Utajuaje ni upande upi wa kipande cha kiazi mviringo una chumvi chumvi zaidi?’’
  • Mtu wa pili kauliza “Hivi unaweza ukapunguza uzito kwa kujisugua kwa upole juu ya tumbo?”
INAYOHUSIANA  Ijue Spark 2 simu mpya kutoka Tecno

Kazi kweli kweli lakini Aaaah! Tuachane na hayo. Leo TeknoKona itakupa jibu juu ya kama chaja fupi inachaji kifaa chako kwa uharaka kuliko ile ndefu au la.

JIBU

Ingekuwa tunaongelea kuhusu Server za kompyuta jibu lingekuwa ni kweli. Kwamba server ambazo zipo karibu na mahali ulipo zina uwezo wa kutuma taarifa haraka sana na ukazipata kuliko zile ambazo ziko mbali nawe. Hii inaingia akilini kwa kuwa umbali kati ya server hizo na wewe unaweza ukawa ni maelfu na maelfu ya kilomita kwa urefu. Lakini vipi kuhusu chaja za simu?

INAYOHUSIANA  Huduma za Google kwenye Renault, Nissan na Mitsubishi

Upinzani (Resistance) ni kitu ambacho kinajitokeza wakati tunachaji vifaa vyetu. Na katika Fisikia kanuni ya ‘Resistance’ (upinzani) ni Upinzani = Urefu / Eneo (Resistivity = Length / Cross Sectional Area)

Kampuni Ya Upinzani (Resistivity)
Kanuni Ya Upinzani (Resistivity)

Kulingana na kanuni hiyo inamaanisha kuwa kama upinzani ukiwa ni mkubwa sana basi hata kifaa chako kitachukua muda mrefu kujaa chaji

‘developer’ mmoja katika Forum ya Xda alifanya uchunguzi wa kina juu ya jambo hili. Alilinganisha chaja tatu, 12’’, 13’’ na 72’’

Sasa jinsi ya moto mwingi unavyopita katika chaja ndivyo kifaa chako kinapoweza jaa chaji kwa haraka sio?…. lakini ngoja tuone chaja hizi zilifanyaje kwanza

Alitumia chaja mbili ya kwanza ilikuwa ni Samsung ya Amps 2 na ya pili ilikuwa ni Asus yenye Amps 1.35.

INAYOHUSIANA  Programu tumishi 46 zaondolewa kwenye Google Playstore
Ukweli Juu Ya Chaja Ndefu Na Fupi, Ipi Kasi Kubwa Katika Kujaza Chaji Katika Kifaa
Ukweli Juu Ya Chaja Ndefu Na Fupi, Ipi Kasi Kubwa Katika Kujaza Chaji Katika Kifaa

Unaweza ukaona kuwa chaja 12’’ inachaji kifaa haraka kuliko ile ya 36’’ na 72’’. Lakini kwa kuangalia katika chaja ya Asus inaonyesha kuwa chaja ile ya 12’’ haina utofauti mkubwa sana na ile ya urefu wa 36’’

Ni kweli basi kuwa chaja zenye urefu mdogo zinaingiza chaji kwa haraka kwenye vifaa vyetu kuliko zile zenye urefu mkubwa.

Je na wewe una swali ambalo ungependa ujibiwe? Tuandikie hapo chini sehemu ya comment na sisi tutakujibu

Kwa maujanja, habari na mambo mbalimbali tembelea mtandao wako pendwa wa TeknoKona kila siku. Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share
Tags: ,

Hashdough

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com