fbpx

simu

Unataka Kuuza Simu? Fanya Haya Kwanza!

unataka-kuuza-simu-fanya-haya-kwanza

Sambaza

Maswali yanaweza yakawa ni mengi sana juu ya simu yako ya zamani wakati ukiwa umepata simu mpya sio? .. wengi huwa wanafikiria kugawa na wengine kuuza simu hizo. Hakuna chaguo sahihi na chagua ambalo sio sahihi kwani itategemea na matakwa ya mmiliki wa kifaa hicho.

Lakini tuchukulie kwamba unataka kuuza simu janja yako ya zamani lakini cha msingi kujua hapa ni kwamba hutapata kiasi ambacho ni sawa sawa na ulichonunulia simu hiyo.. mfano simu janja ulinunua shilingi hamsini usitegemee baada ya kuitumia bado utaweza iuza kwa bei hiyo hiyo.

Cha msingi hapa ni kwamba, jitahidi kadri ya uwezo wako katika kutunza kifaa hicho, hii itasaidia simu janja hiyo ibaki katika hali nzuri ambayo itakuwezesha kuiuza kwa bei ambayo ina unafuu, tofauti kabisa na simu ikiwa imechoka!

Sawa Umeshakua Maamuzi Kwamba Unauza Simu janja Yako, Chukua Hatua Hizi Basi……

  1. Tambua/Jua Thamani Ya Simu Hiyo
SOMA PIA  Galaxy Note Fan Edition: Samsung yatumia sehemu ya Note 7 kuunda simu mpya

Thamani ya simu hiyo katika hali yake unaweza kuijua kwa kufanya uchunguzi kidogo. Ulizia sehemu mbalimbali kwanba simu iliyotumika katika hali hiyo inaweza uzwa kwa kiasi gani. Njia ya haraka kabisa ni kuingia katika mtandao na kuanza kuulizia simu hiyo. Utapata ufumbuzi mwingi hii ni ikiwepo na bei ya kuuza simu janja hiyo.

Mitandao kama eBay, kupatana na mingine mingi itakusaidia sana katika kuhakikisha unapata bei ya simu janja husika, kulingana na hali ambayo kipo nayo.

     2. Amua Namna Ya Kupokea Malipo

SOMA PIA  Fununu kuhusu Google Pixel 4a

Je unataka kulipwa vipi? je simu hiyo utaiuza mtandaoni au biashara itafanyika ana kwa ana? ni mambo ya msingi sana ya kujiuliza kabla ya kuendelea na zoezi la kuuza simu hiyo. Ukishajua kuhusiana na yote vile vile kumbuka kuwa mnunuzi nae anaweza kagua simu hiyo na bado akaja na bei yake ambayo anapendezwa nayo kuuziwa (kulingana na hali ya simu hiyo).

Kabla ya hatua hii kumalizika vile vile  ni muhimu sana kwa pande zote mbili kukubaliana vigezo na masharti kwenye biashara hiyo, vitu kama urejeshaji wa simu (mteja akishanunua) na mambo mengine yote ya muhimu inabidi yaongelewe na pande zote mbili.

3. ‘Back Up’ Na Kisha ‘Reset’ Simu

SOMA PIA  Thamani ya kava la simu ya Messi ni 50M za kitanzania!

Kama katika simu hiyo kutakua na vitu vyako vya msingi kama vile namba za simu, picha n.k unaweza ukazihifadhi mtandao kwa njia kama hizi  baada ya hapo zoezi linalofuata ni kufuta kila kitu katika simu hiyo. Hili lina fahamika kama ‘Reset’ ili kuirudisha katika hali yake ya mwanzo kabisa.

Mambo ya Kufanya Kabla ya Kuuza au Kubadilisha Simu Yako
Mambo ya Kufanya Kabla ya Kuuza au Kubadilisha Simu Yako

Mpaka hapo natumai utakua ushajua ni vitu gani vya muhimu vya kuzingatia ukiwa unataka kuuza simu yako. ningependa kusikia kutoka kwako, unadhani ni kitu gani cha muhimu ambacho hakijaandikwa hapo juu?

Niandikie kwenye sanduku la maoni hapo chini, pia usisahau kutembelea mtandao wako namba moja wa TeknoKona kwani daima tupo nawe katika teknolojia.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Sambaza
Tags:

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

    Toa Maoni

    Your email address will not be published. Required fields are marked*