fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Samsung simu Teknolojia

Unafahamu nini kuhusu simu janja Samsung Galaxy A22 4G?

Unafahamu nini kuhusu simu janja Samsung Galaxy A22 4G?

Spread the love

Samsung imeshazindua simu janja za uwezo wa kati kadha wa kadha lakini haijafikia mwisho kwani karibu miezi miezi miwili iliyopita walizindua Galaxy A22 4G.

Makampuni mengi (kama si yote) yanayofanya biashara ya simu janja yamekuwa yakijitahidi kutoa rununu ambazo zinalenga watu wenye vipato tofauti halikadhalika wale ambao hawapendi matumizi makubwa kwenye simu janja hizi rununu zenye uwezo wa kawaida wanazipenda pia.

SOMA PIA  Vijana Watanzania waleta Soka ya Ligi Kuu Tanzania kwenye SImu!

Samsung Galaxy A22 4G ni simu janja ambayo inaangukia kwenye kundi la rununu ambazo uwezo wake si wa juu wala chini bali katikati kutokana na kile ambacho kimewekwa ndani yake. Sifa zake ni hizi:

Kioo :
 • Ukubwa: inchi 6.4
 • Ubora: Super AMOLED (720*1600px, 90Hz); ung’avu wa hali ya juu sana+ kamera ya mbele imeingia kwa ndani kidogo mithili ya bonde la ufa
Kamera :
 • Kamera Kuu: MP 48, 8 na mbili zina MP 2+taa moja ya kuongeza mwangaza sehemu ambazo kuna mwanga hafifu. Ina uwezo wa kurekodi picha mnato za ubora wa 1080px
 • Kamera ya Mbele: MP 13+Ina uwezo wa kurekodi picha mnato za ubora wa 1080px
Betri/Chaji :
 • Li-Ion 5000 mAh
 • USB-C 2.0, OTG+uwezo wa kuchaji haraka kwa nguvu ya 15W
  Galaxy A22

  Simu hii ina teknolojia ya 4G LTE, spka ya nje ipo. Teknolojia ya kutumia alama ya kidole imewekwa kwa pembeni(kwenye kitufe cha kuzima/kuwasha simu), inatumia Bluetooth 5.0, WiFi. Uso wa mbele unalindwa na kioo kigumu na upande wa nyuma ni plastiki.

   

Kipuri mama :
 • MediaTek Helio G80
Uzito :
 • Gramu 186

Programu Endeshi

 • One UI 3.1, Android 11
Rangi :
 • Nyeupe, Nyeusi, Udhurungi
  Galaxy A22

  Simu hii ipo katika toleo mbili tofauti; kuna moja inatumia kadi moja ya simu na nyingine ina uwezo wa kuweka laini mbili. Ina sehemu ya kuchomeka spika za masikioni lakini haina NFC.

   

Bei yake inaazia $205|zaidi ya Tsh. 471,500 (4/64), $249.99|zaidi ya Tsh. 574,977 (4/128) na $251.60|zaidi ya Tsh. 578,680 (6/128) kwa gharama za ughaibuni na tayari ipo sokoni. Kumbuka kufuatilia TeknoKona ili uweze kuhabarika halikadhalika kuelimika kuhusu teknolojia.

Vyanzo: GSMArena, mitandao mbalimbali

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania