fbpx
CocoFax, Gmail, Google, Teknolojia

Unafahamu nini kuhusu CocoFax?

unafahamu-nini-kuhusu-cocofax
Sambaza

Teknolojia imekuwa bora kila leo na bado na haijaishia hapo kwani hadi leo hii kuna mashirika, taasisi matumizi ya kipepeshi ni nyenzo ya kufanikisha ufikishaji wa taarifa kutoka sehemu moja hadi nyingine.

Katika dunia ya leo pengine kuna watu wamesahau kutumia kipepeshi na hii imesababishwa na ukuaji wa teknolojia kitu ambacho kinasababisha watu kuachana na matumizi ya kipepeshi katika kufanikisha kutuma nyaraka mbalimbali lakini je, nikuulize umesikia kuhusu CocoFax?

CocoFax ni teknolojia isiyohitaji mashine (kipepeshi), wino kuweza kumuwezesha mtu kutumia nukushi na kumfikia husika. Huduma hii inafanya kazi kwenye Gmail.

Hatua za kufuata ili kuweza kutuma nyaraka kwa njia ya nukushi kwenye Gmail

>Inabidi kufungua akaunti ya CocoFax kwa majaribio katika kipindi cha siku 30 KUPITIA HAPA lakini kumbuka kutumia barua pepe yako ya Gmail,

INAYOHUSIANA  Axon M: Simu janja yenye vioo viwili kutoka ZTE

>Ukishafungua kaunti ya CocoFax, nenda kwenye uwanja wa kuandika ujumbe ndani ya Gmail kisha kwenye sehemu ya kuandika anwani ya unayetaka kumtumia kitu anza na namba ya utambulisho wa nchi+nukushi+@cocofax.net (mfano 25522458….@cocofax.net),

>Utaandika ujumbe pamoja na kuambatanisha nyaraka unazotaka kuzituma kwenda kwa mhusika kama kawaida. KUMBUKA: Nyaraka ambazo unaweza kuambatanisha na kuzituma katika mfumo wa nukushi klwenye Gmail ni PDF, jpg, jpeg, png, doc, docx, xls, xlsx, na tiff .

Cocofax
Google yaanzisha mfumo wa kutumia nukushi kwenye Gmail.

>Mara baada ya kutuma utapokea taarifa kuwa ujumbe wako umemfikia mhusika lakini pia iwapo kutakuwa kuna kitu kimekosewa na kusababisha kile ulichokituma kutofika kwa mlengwa utajulishwa pia ili kuweza kurekebisha na kutuma tena.

INAYOHUSIANA  Apple yathibitisha kuwa inatengeneza magari.

Hakuna tofauti wa mfumo wa kupokea jumbe za CocoFax kwenye Gmail; vitu vipo vilevile kama ambavyo tunafanya mawasiliano kwa njia ya barua pepe. Kilichokigeni hapa ni anwani inayotumika ili kuwezesha ujumbe kufika lakini pia teknolojia yake isiyohitaji kipepeshi kufanikisha lengo.

Kipepeshi ni nini? Hii ni mashine inayotumika kutuma nyaraka kwa njia ya nukushi (fax number).

Cocofax
Hiyo ndio kipepeshi; teknolojia ambayo bado inatumiwa mpaka hivi leo.

Matumizi ya CocoFax ni BURE katika kipindi cha siku 30 za mwanzo kisha baada ya hapo mtumiaji atalazimika kulipa $12.99 kwa mwezi kupata huduma hiyo. Je, unajiona ukihama kutoka kwenye matumizi ya kipepeshi kuja kwenye CocoFax?

Vyanzo: Android Police, CocoFax

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|