Mara zote tunaponunua kompyuta tunakuta tayari hard disk imeshagawanywa mara 2 au zaidi kulingana na ujazo wa kihifadhi data hicho lakini je, ulishawahi kujiuliza kwanini HardDisk zinagawanywa (partitioned)? Karibu uweze kujua.
Nini maana ya ‘partitioning‘?
Hii inamaanisha kitendo cha kuigawanya kifaa cha kuhifadhi data kwenye kompyuta yako kinawezesha kuigawanya hard disk ya kompyuta yako mara nyingi utakavyo kulingana na ujazo wa Hard disk lakini daima programu endeshaji hukaa kwenye Local disk C.
Kwanini ni muhimu kugawanya kihifadhi data cha kompyuta?
Zipo sababu nyingi ambazo hufanya wataalamu wa mambo ya kompyuta (kama mimi, haha!) kunafanya partition kwenye kompyuta kabla ya kuweka programu endeshaji. Hizi hapa ni baadhi ya sababu kuu zinatufanya tuigawanye hard disk:
- Kufanya data zako kuwa katika mpangilio mzuri. Ni ukweli usiopingika kuwa iwapo hard disk yako imegawanywa basi data zako zitakuwa katika mpangilio mzuri kwani mafaili yanayohusiana na OS pamoja na programu nyingine wezeshaji yatakuwa katika partition yake huku data nyingine zikiwa kwenye partition tofauti; yaani Local disk C, D na nyinginezo.
- Urahisi wa kufanya recovery. Pale ambapo kihifadhi data kinapokuwa kimepata majanga na iwapo hard disk ya kompyuta yako ilikuwa imegawanywa basi itakuwa rahisi kupata (recover) data zako pindi pale kifaa hicho kitakapokuwa shwari baada ya kutengenezwa. ‘Back up’ ya programu endeshaji yako hakikisha kwenye mipangilio (settings) huwa inahifadhiwa kwenye partition (uhifadhi) mwingine kama vile D.
- Usalama wa data zako kuongezeka. Hard disk ambayo imeshagawanywa data ambazo zinahifadhiwa humo huwa salama zaidi. Kumbuka kama umeigawanya basi local disk C utaitumia kwa ajili ya kutunza programu endeshaji na programu wezeshaji wakati local disk D ndio utahifadhi mafaili yako. Hivyo hata kama programu endeshaji ikaathirika iwe kwa virusi, umeme kupita mwingi/kidogo na kusababisha kompyuta kuzima ghafla, n.k bado utaweza badili programu endeshaji na bado ukafanikiwa kupata data zako zote zilizopo kwenye diski D.
Ni matumaini yetu kuwa umeweza kujua umuhimu wa hard disk yako kugawanywa na daima usikubali kutumia kompyuta ambayo hard disk yake haijagawanywa. Tupe maoni yako tafadhali.
Vyanzo: Ujuzi binafsi pamoja na mitandao mbalimbali
One Comment
Comments are closed.