fbpx

Android, apps, Chrome, Intaneti

Ulinzi waboreshwa kwenye Chrome ya simu

ulinzi-waboreshwa-kwenye-chrome-ya-simu

Sambaza

Moja ya kivinjari ambacho watumiaji wengi wa simu janja wanakitumia ni Google Chrome na ni wazi kuwa kutokana na ukuaji wa teknolojia uhalifu wa kwenye mtandao nao pia umeshika kasi jambo ambalo linafanya makampuni kuboresha ulinzi kwenye bidhaa za kidijiti wanazozimiliki.

Watu wengi ambao wanapenda kupata kile wanachokitafuta huwa wanperuzi tuu kwa kutumia kivinjari ambacho kipo tayari kwenye simu; kama ni rununu ya Android moja kwa moja Chrome inakuwepo ndani na iwapo unatumia iPhone, iPad basi kivinjari cha Safari kinahusika.

INAYOHUSIANA  Namna ya kuweka Play Store katika simu zenye mfumo wa kichina

Katika hali ya kukabiliana na uhalifu unaohusisha mambo ya teknolojia hivi sasa kwenye kivinjari cha Chrome mhusika ataweza kupata taarifa iwapo mtu amejaribu kuweka nenosiri kwenye akaunti isimhusu ili kuweza kuingia ndani. Chrome inatoa taarifa kwa zile huduma zote ulizokubali kivinjari husika kiweze kukumbuka nywila.

Baada ya mhusika kupata taarifa kuwa akaunti yake (nenosiri) ya kwenye huduma fulani kuna mtu amejaribu kuitumia hapohapo atakuwa na uwezo wa kuangalia na kuweza kubadilisha nywila kwenye huduma husika. Katika kufanikisha hili Chrome inatuma taarifa kuhusu jaribio la kuingia kwenye akaunti kwenda Google katika muundo wa kuficha (encrypted) ambapo anayepokea taarifa (Google) anakuwa hajui jina maalum (username) na nywila ya mhusika.

Chrome ya simu
Chome ya kwenye iOS/Android yaboreshwa: Sasa itakupa taarifa iwapo mtu mwingine amejaribu kuingia kwenye akaunti yako na kukushauri uiangalie ikiwezekana ubadilishe nenosiri; inaweza kuwa ya Facebook, Twitter, n.k.

Yanayokuja kwenye Chrome ya simu

Katika siku za usoni mtu ataweza kuangalia iwapo nenosiri la akaunti yake kenye huduma fulani imejaribiwa kutumiwa na mtu mwingine kupitia “Safety check” na iwapo kipengele cha “Safe browsing” kimeruhusiwa bila kusahau kuwa toleo la karibuni kabisa. Kwenye iOS watu wataweza kutumia kipengele cha barua pepe (jina maalum) na nywila kujijaza zenyewe kitendo hicho kitahitaji kuthibitishwa kwa alama ya kidole, sura kabla ya kufanyika.

INAYOHUSIANA  Mambo yanayokera katika makundi ya WhatsApp
Chrome ya simu
Chrome ya kwenye iOS mbioni kutumia alama ya kidole, uso ili kuruhusu barua pepe/nywila kujijaza zenyewe kuingia kwenye akaunti fulani.

HIvyo ndivyo ulinzi unavyozidi kuboreshwa ili kukabiliana na wale ambao wanapenda kuingia kwenye akaunti za watu jambo ambalo linahatarisha faragha ya mtu mtandaoni.

Vyanzo: Gadgets 360, GSMArena

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Sambaza

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

    Toa Maoni

    Your email address will not be published. Required fields are marked*