fbpx
Android, Intaneti, iOS, Maujanja, simu, Teknolojia, Usalama, whatsapp

Ulinzi wa akaunti yako ya WhatsApp ni muhimu

ulinzi-wa-akaunti-yako-ya-whatsapp
Sambaza

Programu tumishi ya WhatsApp kwa muda mrefu imetoa fursa kwa watumiaji wake kuweza kuweka ulinzi wa ziada kwenye akaunti zao kwa njia inayofahamika kama Two-step verification.

Njia hii inakuwezesha kwa akaunti yako kuwa salama zaidi hata pale mdukuaji anajaribu kufungua akaunti yako kwa kutumia laini yako ya simu itamlazimu kuingiza nywila ambayo wewe uliiweka katika akaunti yako hapo awali.

Namba za siri (nywila) utakazoingiza zitakuwa tarakimu sita (6) tu ambapo utaingiza mara mbili kuthibitisha na pia utaweka barua pepe yako itakayokusaidia pindi utakaposahau nenosiri. Ujazaji wa nywila utakuwa wa mara kwa mara baada ya siku kadhaa ili kukusaidia kuendelea kukumbuka.

Pale unapofuta programu tumishi ya WhatsApp au kujaribu kuweka kwenye simu nyingine hapo lazima utalazimika kuweka nywila yako.

Na hii ndio njia salama kwa akaunti ya kutoweza kudukuliwa na mtu mwingine ambae hataijua nywila yako isipokuwa wewe mwenyewe, hivyo zoezi lake la kutaka kudukua kushindikana.

Leo kupitia teknokona tutakuelekeza kwa njia rahisi zaidi kufanikisha hilo na namna ya kuwezesha fuata hatua zifuatazo hapo chini:-

INAYOHUSIANA  Marufuku kurusha ndege zisizo na rubani/Drones Saudi Arabia

1. Fungua akaunti yako ya WhatsApp. Angalia upande wa kulia kwenye vidoti vitatu na ufungue hapo kisha nenda Settings>> Account>>Two-step verification>>Enable
ulinzi wa akaunti yako

2. Jaza nenosiri (nywila) lako ambazo zinatakiwa tarakimu sita tu utakazopenda kisha utarudia tena kuweka namba hizo hizoulinzi wa akaunti yako3. Utajaza barua pepe yako na kuirudia tena katika kipengele kitakachofuata halafu utabonyeza save.ulinzi wa akaunti yako4. Mwisho kabisa utabonyeza “Done“.

INAYOHUSIANA  Madhara ya kulala na Simu yako ikiwa Imewashwa

ulinzi wa akaunti yako

Kwa hatua hizo utakuwa umewezesha kutengeneza ulinzi kwenye akaunti yako ya WhatsApp yako kutoweza kudukuliwa na mtu mwingine. Endelea kufuatilia tovuti yako ya teknokona kwa taarifa na mbinu mbalimbali.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share
Tags: , , ,

Siyan

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.